Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Edward Mpogolo amewataka Walimu wazalendo kuhakikisha wanasimamia maadili ya wanafunzi kuanzia suala la nidhamu, mavazi pamoja na ufaulu ili watoto waweze kukua katika misingi bora.
Mhe. Mpogolo ametoa maagizo hayo katika Kongamano la Jukwaa la Walimu Wazalendo Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam lililofanyika katuka Ukumbi wa Shule ya Sekondari Shaaban Robert sambamba na kaulimbiu isemayo 'Wazalendo tunasimama na Mama, uzalendo kwa vitendo'.
Aidha, Mhe. Mpogolo ameeleza kuwa ili walimu waonyeshe uzalendo ni lazima wasimamie maadili kwa wanafunzi wao pamoja na kuhakikisha wanawalea wanafunzi hao katika misingi bora bila kusahau suala la utunzaji wa mazingira, elimu ya kupinga rushwa pamoja na elimu ya lishe.
“Wanafunzi wengi siku hizi hawana maadili kwani wanaambatana na makundi yasiyofaa hivyo tunaamini mwalimu mzalendo atakwenda kusimamia maadili ya watoto Shuleni ambayo yatamfanya mwanafunzi kusoma kwa bidii na hivyo ufaulu kuongezeka kwa kasi zaidi, hivyo ni jukumu lenu kama Wazalendo kuyabeba haya na kuyatekeleza kwa manufaa ya nchi yetu”.
Kwa upande wake Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam Mhe. Omary Kumbilamoto ameeleza kuwa Serikali imefanya makubwa katika kipindi cha muda mfupi ambapo Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameendelea kuimarisha sekta ya elimu kwa kujenga madarasa ya ghorofa ambayo yameweza kuondoa msongamano wa wanafunzi darasani na kuahidi kushirikiana na walimu.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Anuani ya Posta: S.L.P 20950
Simu ya mezani: 0738 378 386
Namba ya Mkononi: 0738 378 386
Barua Pepe: info@dcc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.