Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Edward Mpogolo leo Julai 18, 2023 amezindua zoezi la Upimaji Afya Bure katika Viwanja vya Mashujaa (Jirani na Kituo cha daladala cha Mnazi Mmoja) ambapo Wakazi wakazi wa Wilaya ya Ilala watapata Fursa ya kupima magonjwa bure chini ya madaktari bingwa.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Mhe. Mpogolo amesema lengo la kampeni ni kuwafikia wananchi wengi zaidi na ni fursa pekee kwa wasio na bima za afya, watoto yatima pamoja na wananchi wote wasio na uwezo kuhudumiwa bure.
"Katika zoezi hili madaktari bingwa kutoka Hospitali na Taasisi za Afya mbalimbali watahudumu zikiwemo Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete, Taasisi ya Mifupa MOI, Hospitali ya Taifa Muhimbili, CCBRT, MSD, MDH, na Zenufa Laboratories hivyo tujitokeze kwa wingi kutumia fursa hii adhimu na ya kipekee ya kuimarisha afya zetu." Ameongeza Mhe. Mpogolo.
Zoezi la Upimaji Afya Bure la Afya Check litafanyika kwa siku mbili (18 Julai 2023 na 19 Julai 2023) kwenye Viwanja vya Mashujaa na Huduma zitazopatikana ni upimaji wa Meno, Macho, Magonjwa ya Wanawake, Watoto, Presha, Moyo pamoja na uchangiaji wa damu.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Anuani ya Posta: S.L.P 20950
Simu ya mezani: 0738 378 386
Namba ya Mkononi: 0738 378 386
Barua Pepe: info@dcc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.