Katika kuendeleza juhudi za kidiplomasia za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo tarehe 21 Julai 2025, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Albert Chalamila, amekutana na Meya wa Dallas, Mhe. Eric L. Johnson, katika ofisi yake iliyopo Ilala Boma, jijini Dar es Salaam.
Meya wa Dallas Mhe. Johnson amepokewa na mwenyeji wake Mhe. Omary Kumbilamoto, Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam pamoja na Mkurugenzi wa Jiji Ndg. Elihuruma Mabelya wakiambatana na Viongozi mbalimbali kutoka katika Ofisi ya Wizara ya Mambo ya Nje, Ubalozi wa Marekani, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam na Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam.
Lengo la mkutano huo lilikuwa kujadili maeneo ya kimkakati ya ushirikiano baina ya Dar es Salaam na Dallas, ikiwa ni pamoja na biashara, uwekezaji, na maendeleo ya kiuchumi.
Ujio wa Meya Johnson si tu ishara ya urafiki, bali pia ni fursa mpya ya kuimarisha mahusiano ya moja kwa moja kati ya miji hiyo miwili, katika nyanja zinazogusa maisha ya wananchi na ustawi wa miji.
Dar es Salaam inaendelea kujidhihirisha kama lango la fursa Afrika Mashariki, huku ikiwakaribisha wadau kutoka mataifa mbalimbali duniani.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Anuani ya Posta: S.L.P 20950
Simu ya mezani: 0738 378 386
Namba ya Mkononi: 0738 378 386
Barua Pepe: info@dcc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.