Diwani wa Kata ya Gongolamboto Mhe. Lucas Rutainurwa leo Septemba 30, 2023 amefungua jengo la ofisi ya Serikali ya Mtaa Ulongoni-A lenye thamani ya shilingi milioni 19.4 fedha ya Mkuza wa bomba la gesi (TPDC), Mfuko wa Jimbo pamoja na fedha kutoka kwa wahisani mbalimbali.
Akiongea kwa niaba ya Waziri wa Ardhi Mhe. Jerry Silaa (Mb), Diwani wa Kata ya Gongolamboto Mhe. Lucas Rutainurwa amesema “Nipende kutoa Shukrani zangu kwa Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Ulongoni - A kwa kazi Nzuri aliyoifanya ya kusimamia ujenzi huu bila kuwasahau wadau wote wa Maendeleo waliochangia kukamilika kwa ujenzi huu ikiwemo Ofisi ya Mbunge Jimbo la Ukonga pamoja na Mkuza wa bomba la gesi ( TPDC) kwani wadau hawa wameonesha juhudi kubwa sana za kuchochea maendeleo ya nchi yetu kwani maono ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ni kuona wadau wanakua chachu ya kuchochea Maendeleo ya nchi yetu”.
Aidha Mhe. Lucas ametoa wito kwa Wenyeviti wa Serikali za Mitaaa mingine kuhakikisha wanafanya kazi kwa uadilifu na uwajibikaji lengo likiwa ni kuhakikisha Wananchi wanapata huduma muhimu kwa wakati.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam Bi. Tabu Shaibu amewashukuru viongozi wa Serikali za Mitaa kwa uwajibikaji walioufanya hadi kukamilisha ujenzi wa jengo la Serikali ya Mtaa wa Ulongoni A huku akiwahakikishia Ofisi ya Mkurugenzi kutekeleza ipasavyo yote waliyoomba.
“Kutokana na uwajibikaji wenu mliouonesha katika kukamilisha ujenzi wa ofisi hii ni dhahiri kwamba fedha takribani milioni 20 zilizotengwa kwaajili ya ukamilishaji wa jengo hili zitatumika vyema kulingana na matumizi hivyo tuendelee kulipa kodi kwa Maendeleo ya Halmashauri yetu na nchi kwa ujumla”.
Sambamba na hilo Bi. Tabu Shaibu amewakumbusha Wananchi wa Mtaa wa Ulongoni A kufika ofisi za Kanda namba tano zilizopo Kata Gongolamboto kwani huduma zote zinapatikana katika ofisi hizo ikiwemo utoaji wa leseni, vibali vya ujenzi pamoja na huduma nyingine muhimu.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa Ulongoni A Bw. Abraham Munisi Ameeleza kuwa “Ofisi hii ya Serikali ya Mtaa imetekeleza kwa Fedha takribani shilingi bilioni 19.4 kutoka kwa wadau mbalimbali pia nipende kutoa shukrani zangu kwa Mkurugenzi wa ABC Capital kwa kutuachia jengo lake kwa miaka 8 bila kutudai kodi huku mwananchi Oes Nyasi akitoa eneo lake mwaka 2009 kwaajili ya ujenzi wa Serikali ya Mtaa hii inaonyesha jinsi gani wadau wa maendeleo wanavyounga mkono jitihada za Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kukuza uchumi kwa maendeleo ya nchi yetu”.
Sambamba na Hilo Bw. Munisi ameiomba ofisi ya Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam fedha kwaajili ya ukamilishaji wa ofisi kwani Ofisi imebakiza vitu vichache kukamilika.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Anuani ya Posta: S.L.P 20950
Simu ya mezani: 0738 378 386
Namba ya Mkononi: 0738 378 386
Barua Pepe: info@dcc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.