Uongozi wa Kata ya Kipunguni kwa kushirikiana na Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kupitia Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi wameandaa hafla ya Maadhimisho ya Siku ya Chakula Duniani iliyofanyika katika viwanja vya Moshi Bar Kata ya Kipunguni Jijini Dar es Salaam sambamba yenye kaulimbiu isemayo ‘Maji ni Uhai, Maji ni Chakula, hakuna wakuachwa nyuma’ ikiwa na lengo la kuhimiza umuhimu mkubwa wa maji katika ardhi na kuwa maji ni msingi mkubwa katika chakula chetu.
Akizungumza katika hafla hiyo mgeni rasmi ambaye ni Diwani wa Kata ya Kipunguni Mhe. Stephen Mushi ameeleza kuwa “Siku ya chakula duniani imekua agenda muhimu ya kuondoa njaa katika Mataifa kwani siku hii imeendelea kusimamia usala wa chakula Duniani kote hasa wakati wa majanga hivyo baada ya kutembelea mabanda na kujionea namna lishe bora inaneemesha afya nitoe wito kwa Walimu kuhakikisha Shule za Msingi na Sekondari wanaenda kutumia unga wa lishe ili kupunguza hali ya udumavu na uelewa mdogo wa kufikiri kwa Wananfunzi kwani juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni kuhakikisha watoto wanapata mlo kamili kwa afya na ukuaji wa akili zao kwa ujumla.”
Sambamba na hilo Mhe. Mushi alitoa shukrani zake kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kushirikiana na uongozi wa Kata yaKipunguni kuwezesha maadhimisho ya siku ya chakula Duniani ambayo yataenda kuleta mabadiliko kwa jamii.
Awali akiongea wakati wa hafla hiyo Kaimu Mkuu wa Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi Bi. Sije Libe ameeleza kuwa “Maadhimisho haya yanatoa fursa ya kutambua mchango muhimu unaotolewa na wakulima wadogo wadogo, jamii za wavuvi na wafugaji katika maendeleo endelevu na katika kutimiza mkakati wa kutokomeza njaa kupitia mifumo endelevu ya chakula hivyo nitoe wito kwa wananchi msimu huu wa vuli ambao mvua zake ni za muda mfupi muhakikishe mnachagua mbegu zinazostahimili ukame na za muda mfupi ili muweze kupata chakula kani tutapata kuepuka madhara ya lishe duni pindi tutakapozalisha mazao bora na kwa wakati sahihi.”
Siku ya Chakula Duniani huadhimishwa kila tarehe 16 Oktoba ikizingatia suala la njaa na mustakabali wa chakula, watu na Dunia kwa siku zijazo.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Anuani ya Posta: S.L.P 20950
Simu ya mezani: 0738 378 386
Namba ya Mkononi: 0738 378 386
Barua Pepe: info@dcc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.