Halmashauri ya Jiji la DSM imeendelea kupiga hatua katika kudhibiti maambukizi mapya ya VVU na UKIMWI kwani upimaji wa hiari wa Maambukizi ya virusi vya UKIMWI (VVU), umeongezeka Katika Jiji la Dar es Salaam.
Hayo yamebainishwa Leo Mei 03, 2023 Jijini Dar es Salaam katika Ukumbi wa Arnatouglou wakati wa muendelezo wa mafunzo kwa Baraza la Madiwani yenye lengo la kuwajengea uwezo wa namna ya kupambana na maambukizi ya Virusi vya UKIMWI ili kuweza kufikisha elimu kwa Wananchi wao.
Akiwasilisha mada mbalimbali za Hali halisi ya VVU na UKIMWI pamoja na huduma zinazotolewa, Mratibu wa kudhibiti UKIMWI wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Dkt. Aisha Zuheri ameeleza kuwa “Takwimu zinaonesha namna gani Mkoa wa Dar es Salaam umepiga hatua kubwa kwani maambukizi yameweza kushuka mpaka asilimia 4.7 huku Jiji la Dar es Salaam ikifikia asilimia 108.2% ya kufubaza UKIMWI. Pia dadi ya waliopima na kuandikishwa katika kliniki imefikia jumla ya watu 70,261."
Sambamba na hilo Madiwani hao waliweza kufundishwa matumizi sahihi yakutumia kondomu kama njia mojawapo ya kupunguza maambukizi ya Virusi ya UKIMWI.
Kwa upande wake Mratibu wa VVU na UKIMWI Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam (CHAC) Ndg. Barnabas Kisai akiwasilisha mada ya Wajibu na Majukumu ya Kamati ya Kudhibiti UKIMWI ameweza kuwakumbusha Madiwani kuhakikisha wanafuatilia kwa ukaribu zaidi Kamati za Kata kutekeleza majukumu yao ili kuhakikisha elimu zinawafikia wananchi na maambukizi kupungua zaidi ya hapo awali.
Naye Mwenyekiti wa Baraza la Watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWI Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam (KONGA) Bw. Emmanuel Reubent Msinga, ameishukuru Serikali kwa kuwajali wanaoishi na virusi vya Ukimwi kwani kupitia mikopo ya asilimia 10% ya mapato ya ndani ya Halmashauri kiasi cha shilingi kimetolewa kwaajili ya kuwasaidia Waviu kwaajili ya kufanya shughuli mbalimbali za kiijamii.
“Tunaishukuru Serikali inayoongozwa na Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa kutujali sisi watu tunaoishi na virusi vya UKIMWI kwani kupitia mkopo wa asilimia 10% za mapato ya ndani ya Halmashauri vikundi 5 vimeweza kupewa mkopo wa shilingi ambao husaidia kutekeleza miradi mbalimbali tuliyoianzisha na kuhamasisha wanafunzi namna ya kujikinga na maambukizi ya Virusi vya UKIMWI hivyo kwa niaba ya wanakonga wenzangu tutahakikisha tunashirikiana na serikali katika mapambano dhidi ya UKIMWI.” ameeleza Bw.Msinga.
Akifunga mafunzo hayo Naibu Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Mhe. Ojambi Masaburi amesema “Nipende kuwashukuru wawezeshaji wote mliowezesha mafunzo haya pamoja na madiwani wote mlioshiriki katika mafunzo hayo kwani elimu mliyopewa ni kubwa sana na niimani yangu mtapeleka elimu kwa Wananchi wetu na maambukizi yatazidi kupunguza kwa asilimia kubwa zaidi.”
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Anuani ya Posta: S.L.P 20950
Simu ya mezani: 0738 378 386
Namba ya Mkononi: 0738 378 386
Barua Pepe: info@dcc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.