Katika kutekeleza agizo la Serikali la kufanya usafi kila mwisho wa mwezi pamoja na kuendeleza na kutekeleza Kampeni ya Safisha, Pendezesha Dar es Salaam, leo Oktoba 28, 2023 Viongozi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam wameshiriki zoezi la usafi katika Kanda namba 1 na namba 2 ambapo kwa upande wa Kanda namba 1 usafi umefanyika kwenye Barabara ya Kalenga/Mindu huku Kanda namba 2 usafi ukifanyika kuanzia Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Soko la Machinga Complex pamoja na Barabara ya Kawawa maeneo ya Reli ya Kisasa ya SGR.
Zoezi hilo lililoongozwa na Mkuu wa Kitengo cha Udhibiti Taka na Usafi akiambatana wakuu wa Kanda, Meneja wa Soko la Machinga Complex, Watumishi kutoka Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, wadau mbali mbali wa usafi wakiwemo Wejisa Company Limited , Kajenjere Trading Company Limited, Sateki Trading Limited, Umoja wa wafanyabiashara biashara wadogowadogo maarufu kama machinga pamoja na Wananchi.
Akiongea wakati wa zoezi hilo Mkuu wa Kitengo cha Udhibiti Taka na Usafi Ndg. Rajabu Ngoda amewashukuru wadau wote walioshiriki zoezi la usafi huku akitoa wito kwa wananchi kufanya usafi kama sehemu ya maisha yao ya kila siku kwani mazingira yakiwa safi na afya zetu pia zitakua safi na kuepukana na magonjwa mbalimbali ya mlipuko.
Kwa upande wake Meneja wa Kanda namba mbili Bw. Iddi Lameck ameeleza kuwa “Kama ilivyo ada kila mwisho wa mwezi lazima tufanye usafi katika mazingira yetu hivyo sisi kam kanda baba mbili tumefanya usafi kuanzia Ofisi za Mkuu wa Mkoa Machinga Complex na Barabara ya Kawawa hususani maeneo ya Reli ya Kisasa SGR pia nipende kuwaasa wananchi wafanye usafi kila siku bila kusubiri mwisho wa mwezi ili mazingira ya Jiji letu yawe safi kila siku”.
Naye Meneja wa Soko la Machinga Bi. Stella Mgumia ameshukuru kuanzisha kwa kampeni hii ambayo imefanya Jiji la Dar es Salaam kuwa Safi huku akiwataka viongozi wa Kanda kuwapanga wafanyabiashara wanaoweka vibanda pembezoni mwa barabara katika maeneo yasiyo rasmi kwani viwanda hivyo huwa vinahifadhi takataka nyingi ambazo zinakua kikwazo katika kuthibiti suala la usafi na mazingira ya Jiji letu pia amependekeza kuwa na ushindani wa kila Kanda katika kufanya usafi kwani ushindani huo utapelekea maeneo kuwa safi na mazuri.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Anuani ya Posta: S.L.P 20950
Simu ya mezani: 0738 378 386
Namba ya Mkononi: 0738 378 386
Barua Pepe: info@dcc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.