Na: Shalua Mpanda - Tanga
Timu ya mpira wa miguu kutoka Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam imeibuka na ushindi wa bao 2-1 dhidi ya timu ya Halmashauri ya Mji Handeni Handeni katika mchezo uliozikutanisha timu hizo katika uwanja wa shule ya Sekondari Galanos mkoani Tanga katika mashindano ya SHIMISEMITA.
Alikuwa ni mchezaji wa Timu ya Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam Ernest Tyson aliyepeleka kilio upande wa Handeni mara baada ya kufunga mabao yote mawili dakika ya 23 kipindi cha kwanza na dakika ya 58 ya kipindi cha pili.
Mchezo huo uliokuwa wa kasi na ushindani kwa dakika zote 90 ulianza kwa timu ya Jiji la Dar es salaam kupata goli na goli hilo kudumu hadi dakika 45 za kipindi cha kwanza.
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi na Handeni kufanikiwa kusawazisha goli hilo amabalo halikudumu kwa muda mrefu kabla Tyson kupachika goli la pili ambalo lilidumu mpaka filimbi ya mwisho ya mwamuzi.
Sasa timu ya Jiji inasubiria ratiba inayofuata kufahamu itakutana na timu kutoka halmashauri ipi katika mashindano hayo yaliyoanza rasmi leo Agosti 15 hadi 29 mwaka huu ambapo jumla ya halmashauri 187 zinashiriki.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Anuani ya Posta: S.L.P 20950
Simu ya mezani: 0738 378 386
Namba ya Mkononi: 0738 378 386
Barua Pepe: info@dcc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.