• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Dar es Salaam City Council
Dar es Salaam City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Jiji
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Fedha, Utawala na Utumishi
      • Ujenzi na Zimamoto
      • Udhibiti Taka
      • Mipangomiji, Mazingira na Usafirishaji
      • Afya na Huduma za Tiba
    • Vitengo
      • Mipango, Ufuatiliaji na Takwimu
      • Sheria na Usalama
      • Itifaki, Uhusiano na Umma
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Ugavi na Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Shughuli za Utalii
      • Dar es Salaam Yetu
      • Misitu na Mashamba ya wanyama wafugwao
      • Sehemu za kitamaduni, ngoma za asili na sanaa za mikono
      • Kituo cha Urithi wa Ubunifu Majengo na Utalii
      • Maeneo ya kupumzika, bustani na viwanja vya michezo
      • Maeneo ya Manunuzi
      • Majengo na maeneo ya kihistoria
      • Uwanda wa bahari, fukwe na visiwa
    • Urejelezaji wa Taka Ngumu
  • Huduma Zetu
    • Vibali vya Pikipiki
    • Vibali vya Maegesho ya Teksi
    • Vibali vya Kuingiza Magari ya Mizigo
    • Vituo Vikuu vya Mabasi
    • Udhibiti Taka Ngumu
    • Taarifa za Historia ya Viwanja
    • Mazishi ya miili ya marehemu wasiokuwa na ndugu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha na Uongozi
      • Kamati ya Mipangomiji, Mazingira na Miundombinu
      • Kamati ya Mipango na Ufuatiliaji
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba ya Vikao vya Kisheria
    • Ratiba ya Mstahiki Meya
    • Mameya Wazamani wa Jiji
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi iliyo kwenye Mpango
    • Miradi Inayoendelea
    • Vitega Uchumi vya Jiji
  • Machapisho
    • Sheria
    • Sheria Ndogo
    • Sera
    • Miongozo
    • Taarifa mbalimbali
    • Fomu za Maombi
    • Fomu za Ahadi ya Uadilifu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Hotuba
    • Habari Mpya
    • Matukio

Huduma za Kibiashara kuwafikia wafanyabiashara walipo

Tarehe iliyowekwa: September 18th, 2023

Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kupitia Divisheni ya Viwanda, Biashara naUwekezaji inaendelea kuhakikisha huduma za kibiashara hususani utoaji wa leseni za biashara zinawafikia wananchi kwa wakati na mahali walipo, hayo yamebainishwa leo Septemba 18, 2023 na Mkuu wa Divisheni hiyo wakati wa zoezi la utoaji wa leseni kwa wafanyabiashara wa Kariakoo.

Akiongea wakati wa zoezi hilo litakaloendeshwa kwa mwezi mmoja, Mkuu wa Divisheni ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Bw. Nickas Msemwa ameeleza kuwa Halmashauri ya Jiji la DSM imedhamiria kutoa huduma bora kwa wananchi na kwa ukaribu zaidi kwani wameweza kuanzisha kanda saba za kutolea huduma pamoja na kutoa leseni kwa wafanyabiashara kwa kuwafuata katika maeneo yao ya biashara.

Sambamba na hilo Bw. Msemwa ameesema “Zoezi hili limedhamiria kuwafikia wafanya Wafanyabiashara zaidi ya elfu 15 kwa Kariakoo ambao mpaka sasa wafanyabiashara elfu nane bado hawajapata leseni hivyo mpango mkakati huu wa kuleta huduma karibu yao utasaidia kukamilisha zoezi hili ambapo kwa Kariakoo zoezi hili litaendelea kwa muda wa mwezi mmoja baada ya hapo tutaelekea kanda za pembezoni ila ikumbukwe kuwa utoaji huu wa leseni umeambatana na elimu ya jinsi ya kujisajili kwenye mfumo na namna gani ya kutumia mashine zetu katika utoaji wa risiti hivyo nitoe wito kwa wafanyabiashata wote kutumia fursa hii kujipatia leseni ya biashara papo hapo bila kusubiri na kwa Wafanyabiashara wote wenye taarifa hizi wafike maeneo ya huduma ili wapate leseni zao pamoja na elimu kwa ujumla.”

Akitoa wito kwa Wafanyabiashara wenzake Bw. Julius Joseph Lullenge ametoa shukrani zake kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam pamoja na wataalamu wake kwa kuona tija kuhusu swala la leseni na kuwasogezea huduma hiyo karibu huku akiwahimiza wafanyabiashara wenzake kufika eneo la utoaji huduma na kupata elimu ya namna ya kutumia mashine kwani yeye amefika mahali hapo na ameweza kuelekezwa namna ya kutoa risiti kwa kutumia mashine za EFD na kuweza kuelewa pia ametoa wito kwa wafanyabiashara wenzake kutumia fursa kwa kupata leseni papo hapo na kujifunza kwa ujumla.

Matangazo

  • Bajeti ya Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 June 14, 2023
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI - MTENDAJI WA MTAA (NAFASI 2) July 26, 2023
  • Tangazo la Kuitwa Kwenye Usaili wa kuandika (Mtendaji wa Mtaa) September 19, 2023
  • TANGAZO DHIDI YA UTAPELI WA AJIRA July 20, 2022
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • Naibu Katibu Mkuu Mativila asisitiza ujenzi wa miundombinu bora Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam

    September 22, 2023
  • Mstahiki Meya Halmashauri ya Jiji la DSM Afungua Ofisi ya Mtaa wa Mwanagati

    September 21, 2023
  • Kamati ya Lishe Halmashauri ya Jiji la DSM yafanya Kikao cha kujadili taarifa za utekelezaji wa kazi za Lishe kwa Kipindi cha Robo ya Nne

    September 19, 2023
  • Huduma za Kibiashara kuwafikia wafanyabiashara walipo

    September 18, 2023
  • Angalia zote

Video

NAPA
Video Zingine

Viunganishi vya Haraka

  • Mameya wa zamani wa Jiji
  • Vibali vya kuingia na Pikipiki katikati ya Jiji
  • Udhibiti wa Taka ngumu Jijini
  • Eneo Maalum la Usafi Jijini
  • Kituo cha Urithi wa Ubunifu Majengo na Utalii
  • Uwanda wa Bahari, Fukwe na Visiwa
  • Sehemu za Kitamaduni, Ngoma za Asili na Sanaa za Mikono
  • Majengo na Maeneo ya Kihistoria
  • Maeneo ya Kupumzika, Bustani na Viwanja vya Michezo

Viunganishi Linganifu

  • BUNGE
  • Blogu ya Jiji
  • UTUMISHI
  • IKULU
  • TAMISEMI
  • IDARA YA HABARI MAELEZO

Wasomaji mbalimbali duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM

    Anuani ya Posta: S.L.P 20950

    Simu ya mezani: 2128800

    Namba ya Mkononi:

    Barua Pepe: info@dcc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.