Na Doina Mwambagi
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Mheshimiwa Edward Mpogolo, amesema Wilaya ya Ilala imejipanga kikamilifu kupokea ugeni mkubwa wa marais na viongozi wa nchi za Afrika wanaotarajiwa kuwasili nchini kwa ajili ya mkutano utakaofanyika tarehe 27 na 28 Januari mwaka huu.
Ameyasema hayo leo, tarehe 25 Januari 2025, wakati wa zoezi la usafi wa mazingira lililoongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, eneo la Terminal One.
Mheshimiwa Mpogolo amesema kuwa maandalizi yamefanyika kwa ushirikiano mkubwa kati ya serikali na mashirika binafsi kuhakikisha kila jambo linafanikiwa.
Ameeleza kuwa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam imeweka mkazo mkubwa kwenye usafi wa mazingira ili kuhakikisha jiji linaakisi taswira nzuri ya nchi kwa wageni hao wa heshima.
Aidha, Mkuu huyo wa Wilaya amesisitiza umuhimu wa kushirikiana kwa vitendo katika kufanikisha tukio hilo kubwa.
“Hii ni fursa adhimu kwetu wananchi wa Ilala na Tanzania kwa ujumla. Tunapaswa kuwa mfano wa kuigwa kwa kuwa na ukarimu, usafi, na mshikamano. Hivyo niwaombe kutoa ushirikiano na jeshi la police kuhakikisha usalama na amani vinakuwepo muda wote “ alisema Mheshimiwa Mpogolo.
Mwisho, Mhe. Mpogolo amesema kuwa kwa kusema kuwa hii ni nafasi muhimu ya kuipa Wilaya ya Ilala na Tanzania kwa ujumla nafasi ya kujitangaza kimataifa kama eneo la amani, maendeleo, na mshikamano wa kidiplomasia.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Anuani ya Posta: S.L.P 20950
Simu ya mezani: 0738 378 386
Namba ya Mkononi: 0738 378 386
Barua Pepe: info@dcc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.