Na: Shalua Mpanda - Tanga
Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam imeibamiza Halmashauri ya wilaya ya Monduli kwa seti 25-23 na 25-11 katika mchezo wa mpira wa mikono (Handball) uliofanyika katika viwanja vya Shule ya sekondari Tanga (Tanga Tech) kwenye mashindano ya SHIMISEMITA yanayoendelea mkoani Tanga.
Mchezo huo wa vuta ni kuvute ulioshudia seti ya kwanza iliyokuwa na msisimko wa aina yake baada ya timu zote mbili kuoneshana uwezo ambapo mpaka seti hiyo inaisha Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam ilikuwa inaongoza kwa 25-23.
Seti ya pili timu ya Jiji la Dar es salaam maarufu kama "Dar City'' ilirudi kivingine na kufanya mpaka mwisho wa mchezo huo ubao usome seti 2-0 (25-23,25-11).
Michezo ya SHIMISEMITA inajumuisha michezo mbalimbali ambayo husimamiwa na Shirikisho la Michezo la Halmashauri kwa Serikali za Mitaa na kwa mwaka huu inafanyika katika mkoa wa Tanga.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Anuani ya Posta: S.L.P 20950
Simu ya mezani: 0738 378 386
Namba ya Mkononi: 0738 378 386
Barua Pepe: info@dcc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.