Na: Hashim Jumbe
Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kupitia Idara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji ni moja kati ya washiriki wa maoenesho ya 3 ya uwekezaji na biashara yanayofanyika Mjini Kibaha, Mkoa wa Pwani.
Maonesho hayo yanayofanyika katika viwanja vya stendi ya zamani ya Mailimoja, Mjini Kibaha yalianza tarehe 05 Oktoba, 2022 na kufunguliwa rasmi na Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na yanatarajiwa kufungwa tarehe 10 Oktoba, 2022
Aidha, ushiriki wa maonesho hayo ya wiki ya uwekezaji na biashara kwa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam yanatoa fursa kwa Idara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji kutangaza fursa zinazopatikana ndani ya Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam
"Kwetu sisi Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam maonesho haya yanatupa nafasi ya kutangaza fursa mbalimbali zinazopatikana katika Jiji letu kama vile maeneo ya uwekezaji, huduma za masoko kwa bidhaa mbalimbali za wawekezaji pamoja na wajasiriamali" Bussa Musika, Afisa Biashara
Maonesho hayo ya wiki ya uwekezaji na biashara kwa mwaka huu yamebeba kauli mbiu isemayo 'Pamoja tujenge viwanda kwa uchumi na ajira endelevu'
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Anuani ya Posta: S.L.P 20950
Simu ya mezani: 0738 378 386
Namba ya Mkononi: 0738 378 386
Barua Pepe: info@dcc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.