Na : Doina Mwambagi
Mkurugenzi wa Halmshauri ya Jiji la Dar es Salaam, Ndugu Elihuruma Mabelya, ametoa wito kwa watumishi wa Kanda Namba Moja wa Halmshauri ya jiji la Dar es salaam kuhakikisha wanakusanya mapato ya serikali kwa uadilifu, bila uonevu wala vitisho, kwa kuzingatia haki na sheria.
Ametoa wito huo leo tarehe 23 Mei 2025, wakati wa hafla ya uzinduzi wa Ofisi ya Mkuu wa Kanda Namba Moja iliyofanyika katika Ofisi ya Mtendaji wa Kata ya Upanga Mashariki, jijini Dar es Salaam iliyofanyiwa ukarabati na mdau wa maendeleo kampuni ya "The Car Spa" chini ya Mkurugenzi wake Bw.Khalil Karim
Katika hotuba yake, Ndugu Mabelya amewakumbusha watumishi hao kuwa kazi ya ukusanyaji mapato ni ya msingi katika maendeleo ya jiji, lakini lazima ifanywe kwa uaminifu, heshima kwa wananchi, na kwa kuzingatia misingi ya haki.
“Rushwa, uzembe, uonevu na uvivu ni sumu kwa maendeleo ya jiji letu. Tunahitaji watumishi waaminifu wanaokusanya mapato kwa haki bila kumuonea mtu wala kutumia nafasi vibaya,” amesisitiza Mabelya.
Aidha, amesema kuwa ili jiji lipige hatua, ni lazima kila mmoja atimize wajibu wake kwa uaminifu na uwajibikaji wa hali ya juu, huku akisisitiza umoja na mshikamano ndiyo nguzo ya mafanikio ya pamoja.
Kwa upande wake, Mkuu wa Kanda Namba Moja Kornelio Nnko ameahidi kuongoza kwa weledi na kuhakikisha kuwa mapato yatakusanywa ipasavyo bila manyanyaso, huku akiahidi kushughulikia malalamiko yote yatakayotolewa na wananchi kwa haraka.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Anuani ya Posta: S.L.P 20950
Simu ya mezani: 0738 378 386
Namba ya Mkononi: 0738 378 386
Barua Pepe: info@dcc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.