Na: Shalua Mpanda
Kamati ya Bunge ya Tawala Za Mikoa na Serikali za Mitaa imeonesha kufurahishwa na mradi mkubwa wa uwekezaji wa kituo cha kibiashara cha DDC Kariakoo.
Akizungumza mara baada ya kukagua ujenzi wa jengo hilo la ghorofa sita litakalokuwa na maduka zaidi ya 2000, Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mbunge wa Kilolo Mheshimiwa Justin Nyamoga amesema Mradi huo ni moja ya miradi inayotekelezwa kwa ubia kati ya sekta ya umma na sekta binafsi (PPP).
“Niwapongeze sana Jiji la Dar es Salaam kwa maamuzi sahihi ya kufuata taratibu katika uwekezaji wa PPP, na sisi kama Kamati tunatoa maagizo na maelekezo kwa Wizara ya TAMISEMI kuhakikisha Halmashauri zote zenye fursa zinajifunza kwa Halmashauri ya Jiji la Dsm kuhusu PPP” Alisema Mhe. Nyamoga.
Naye Kamishna wa Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta ya Binafsi Mhe. David Kafulila amezitaka mamlaka zote zenye maeneo yanayoweza kuvuta mitaji ya sekta binafsi,kushirikiana kuvuta Mitaji hiyo.
Jengo hilo lenye thamani ya zaidi ya Shilingi bilioni 33 linalojengwa kwa ubia kati ya Serikali na muwekezaji mzawa kampuni ya TOSHI litakapokamilika litakuwa na maduka takribani na ofisi mbalimbali na litakuwa moja kati ya uwekezaji mkubwa katika Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Anuani ya Posta: S.L.P 20950
Simu ya mezani: 0738 378 386
Namba ya Mkononi: 0738 378 386
Barua Pepe: info@dcc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.