Kamati ya Chakula na Dawa Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam chini ya Mwenyekiti wake Mkurugenzi wa Jiji hilo Elihuruma Mabelya leo hii Septemba 19, 2025 imekutana na kufanya kikao chake cha kwanza kujadili mambo mbalimbali.
Kikao hicho kilichofanyika katika ukumbi wa Mstahiki Meya, pamoja na mambo mengine kimejadili maombi ya wadau mbalimbali walioomba vibali vya kufanya biashara ya duka la madawa ya binadamu (Pharmacy).
Akizungumza mara baada ya kikao hicho, Mwenyekiti Mabelya alisema lengo la Kamati hiyo ni kuwalea na kuwasaidia wadau hao kufanya biashara hiyo kwa kufuata sheria na taratibu zilizowekwa na si kuwakwamisha.
Aidha, amemtaka Mfamasia wa Halmashauri ya Jiji kuhakikisha wanatoa elimu kwa wadau hao ili kuondoa malalamiko kwa wale wenye nia ya kuanzisha biashara hiyo.
"Ni vyema kama kuna taratibu za kufuatwa wajulishwe na kupewa elimu ili kukidhi vigezo vinavyohitajika". Alisisitiza Mabelya
Kwa upande wake Katibu wa Kamati hiyo ambaye pia ni Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Jiji Dkt Frank Chiduo alisema kazi ya Kamati hiyo ni kupitia maombi ya vibali vya kuanzisha maduka ya dawa na kuyapitisha yale ambayo yamekidhi vigezo.
Kamati hiyo yenye wajumbe kutoka Halmashauri ya Jiji wakiwemo Mweka Hazina, Mwanasheria, Afisa Biashara na wengine hukutana kila baada ya miezi mitatu kujadili mambo mbalimbali yanayohusu Dawa na Chakula.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Anuani ya Posta: S.L.P 20950
Simu ya mezani: 0738 378 386
Namba ya Mkononi: 0738 378 386
Barua Pepe: info@dcc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.