• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Dar es Salaam City Council
Dar es Salaam City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Jiji
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Fedha, Utawala na Utumishi
      • Ujenzi na Zimamoto
      • Udhibiti Taka
      • Mipangomiji, Mazingira na Usafirishaji
      • Afya na Huduma za Tiba
    • Vitengo
      • Mipango, Ufuatiliaji na Takwimu
      • Sheria na Usalama
      • Itifaki, Uhusiano na Umma
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Ugavi na Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Shughuli za Utalii
      • Dar es Salaam Yetu
      • Misitu na Mashamba ya wanyama wafugwao
      • Sehemu za kitamaduni, ngoma za asili na sanaa za mikono
      • Kituo cha Urithi wa Ubunifu Majengo na Utalii
      • Maeneo ya kupumzika, bustani na viwanja vya michezo
      • Maeneo ya Manunuzi
      • Majengo na maeneo ya kihistoria
      • Uwanda wa bahari, fukwe na visiwa
    • Urejelezaji wa Taka Ngumu
  • Huduma Zetu
    • Vibali vya Pikipiki
    • Vibali vya Maegesho ya Teksi
    • Vibali vya Kuingiza Magari ya Mizigo
    • Vituo Vikuu vya Mabasi
    • Udhibiti Taka Ngumu
    • Taarifa za Historia ya Viwanja
    • Mazishi ya miili ya marehemu wasiokuwa na ndugu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha na Uongozi
      • Kamati ya Mipangomiji, Mazingira na Miundombinu
      • Kamati ya Mipango na Ufuatiliaji
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba ya Vikao vya Kisheria
    • Ratiba ya Mstahiki Meya
    • Mameya Wazamani wa Jiji
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi iliyo kwenye Mpango
    • Miradi Inayoendelea
    • Vitega Uchumi vya Jiji
  • Machapisho
    • Sheria
    • Sheria Ndogo
    • Sera
    • Miongozo
    • Taarifa mbalimbali
    • Fomu za Maombi
    • Fomu za Ahadi ya Uadilifu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Hotuba
    • Habari Mpya
    • Matukio

Kamati ya Kudhibiti UKIMWI Jiji la DSM yaridhishwa na huduma zinazotolewa kwa WAVIU katika Zahanati ya Mongo la Ndege

Tarehe iliyowekwa: October 31st, 2024

Kamati ya Kudhibiti UKIMWI Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, leo tarehe 31 Oktoba, 2024 imefanya ziara ya kutembelea na kukagua huduma mbalimbali  zinazotolewa kwa Watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWI (WAVIU) lengo likiwa ni kujua changamoto wanazokabiliana nazo ili kuchukua hatua na kuzitatua kwa kipindi cha robo ya kwanza ya Mwaka wa Fedha 2024/2025.

Akiongea wakati wa ziara kwa niaba ya Mwenyekiti wa Kamati ya Ukimwi, Mjumbe wa Kamati hiyo Mhe. Rukia Mwenge amesema “Tunamshukuru Mhe Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha kwa Halmashauri yetu kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya sekta ya Afya ikiwa ni pamoja na vifaa tiba na upatikanaji wa dawa za kufubaza virusi vya Ukimwi kwa urahisi na ukaribu, pia kamati tunawashukuru sana Watumishi wa kituo hiki kwa kujitoa kwenu kuwahudumia na kuwafatilia wagonjwa kwa ukaribu.”

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Halmshauri ya Jiji la Dar es Salaam Dkt. Zaituni Hamza amesema “Zahanati hii inakabiliwa na changamoto ya upungufu wa vyumba za kutolea huduma lakini Halmashauri yetu imetenga milioni 250 kwa ajili ya ujenzi wa jengo jipya katika zahanati yetu. Pia Serikali yetu ya Awamu ya Sita chini ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imesikia kilio chetu kwa kutupatia Watumishi wa Afya wapya 293 watakaosaidia na kupunguza changamoto ya Watumishi katika zahanati na vituo vyetu vya Afya”.

Naye Mratibu wa VVU/UKIMWI Sekta ya Afya Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam (DACC) Dkt. Aisha Zuheri ameeleza kuwa japo Kuna changamoto mbalimbali zinazowakabili pindi wakiwahudumia WAVIU ni matumaini yao Hadi kufikia 2030 kusiwe na maambukizi mapya huku akitoa wito kwa WAVIU kuachana mambo ya tiba mbadala na badala yake kujiwekeza kufata masharti wanayopewa na Wataalamu pamoja na kuzingatia lishe bora Ili kuendelea kutunza Afya zao.

Awali akisoma taarifa ya kliniki ya Tiba na mafunzo ya Zahanati ya Mongo la ndege Dkt. Nuru Kanungila ameeleza kuwa kitengo cha Tiba na mafunzo kilianzishwa mnamo tarehe 08 Aprili, 2013 ikiwa na wateja wa 5 Hadi kufikia wateja 688 ambao wameshawahi kuhudumuwa katika kituo hicho, hata hivyo zahanati inatoa huduma ya upimaji wa virusi vya UKIMWI, kutoa dawa za kufubaza Virusi vya UKIMWI, pamoja kutoa dawa ya kuzuia maambukizi kutoka kwa mama na mtoto na dawa za kifua kikuu.

Matangazo

  • TAARIFA KWA UMMA February 19, 2025
  • TAARIFA KWA UMMA - MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA January 17, 2025
  • MATOKEO YA UPIMAJI WA KITAIFA WA DARASA LA NNE (SFNA) 2024 January 04, 2025
  • UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA, 2025 December 16, 2024
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • "Tutahakikisha tunasimamia Kata 36 na Mitaa 159 ili Jiji la DSM liwe safi" - DC Mpogolo

    May 03, 2025
  • Jiji La DSM laweka mikakati kushinda UMITASHUMTA ngazi ya Mkoa

    April 29, 2025
  • Wakazi wa Jiji la Dar es Salaam waadhimisha Muungano kwa kupanda miti na kufanya usafi wa mazingira

    April 26, 2025
  • Zoezi la usafi wa mwisho wa wiki laendelea

    April 12, 2025
  • Angalia zote

Video

Msimbazi Basin Development Project Implementation Area
Video Zingine

Viunganishi vya Haraka

  • Mameya wa zamani wa Jiji
  • Vibali vya kuingia na Pikipiki katikati ya Jiji
  • Udhibiti wa Taka ngumu Jijini
  • Eneo Maalum la Usafi Jijini
  • Kituo cha Urithi wa Ubunifu Majengo na Utalii
  • Uwanda wa Bahari, Fukwe na Visiwa
  • Sehemu za Kitamaduni, Ngoma za Asili na Sanaa za Mikono
  • Majengo na Maeneo ya Kihistoria
  • Maeneo ya Kupumzika, Bustani na Viwanja vya Michezo

Viunganishi Linganifu

  • BUNGE
  • Blogu ya Jiji
  • UTUMISHI
  • IKULU
  • TAMISEMI
  • IDARA YA HABARI MAELEZO

Wasomaji mbalimbali duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM

    Anuani ya Posta: S.L.P 20950

    Simu ya mezani: 0738 378 386

    Namba ya Mkononi: 0738 378 386

    Barua Pepe: info@dcc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.