Afisa Tawala wa Wilaya ya Ilala Bi. Flora Mgonja, kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Ilala leo 19 Machi, 2024, ameongoza kikao cha Kawaida cha Tathmini ya Utekelezaji wa Mkataba wa Lishe kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Arnatoglou chenye lengo la kupokea na kupitia utekelezaji wa Tathmini ya Hali ya Lishe kwa Ngazi ya Kata kwa robo ya pili (Oktoba - Desemba 2023.)
Akifungua kikao hicho kilichofanyika kwenye ukumbi wa Mikutano wa Arnatoglou, amewataka wajumbe wa kikao hicho kufahamu kuwa lishe ndio msingi wa kila kitu na kwamba kikao hicho ni muhimu katika uboreshaji wa lishe katika jamii na kuwasihi kusimamia afua za lishe kwenye maeneo yao kwa kuzingatia vigezo vya Kitaifa ili kuwa na Jamii yenye afya bora.
Sambamba na hilo, amewasisitiza Wakuu wa Shule za Sekondari na Msingi kuendelea kuhakikisha wanatoa chakula mashuleni ikiwa ni sehemu ya kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ambapo suala la lishe shuleni katika uongozi wa Awamu ya Sita ni kipaumbele.
Awali akieleza mafanikio katika utekelezaji wa viashiria vya lishe vinavyopimwa na Mkataba kwa Ngazi ya Wilaya, Kaimu Mratibu wa Lishe Bi. Neema Mwakasege amesema viashiria vyote 11 vinavyopimwa katika utoaji wa huduma za lishe vimetekelezwa vizuri kwa kufikia kufikia hali nzuri ya utekelezaji, huku mafanikio yaliyopatikana kwenye utekelezaji kwa ngazi ya Kata ni kuimarika kwa ushirikiano kwa ngazi ya vituo, jamii na viongozi wa ngazi mbalimbali toka Wilaya hadi Mitaa pamoja na lishe kuwa swala mtambuka na kuongelewa katika ngazi mbalimbali za vikao katika jamii hasa kupitia watendaji na watoa huduma ngazi ya jamii.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Anuani ya Posta: S.L.P 20950
Simu ya mezani: 0738 378 386
Namba ya Mkononi: 0738 378 386
Barua Pepe: info@dcc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.