Kamati ya Mipango Miji na Mazingira Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, imefanya ziara ya ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo pamoja na usafi wa mazingira karika viwanda ikiwa ni moja ya majukumu ya Kamati hiyo kuhakikisha Jiji linakuwa katika hali ya Usafi, Ziara hiyo ni ya kipindi cha robo ya pili ya mwaka wa fedha 2022/2023 ulioanza Oktoba hadi Desemba 2022.
Wakiwa kwenye ziara hiyo, Kamati iliweza kutembelea na kukagua maeneo mbali mbali yanayosimamiwa na Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam ikiwemo Barabara ya nje katika Soko la Buguruni ambapo hali ya barabara hiyo hairidhishi na inahitaji matengenezo kwani kuna Wananchi wamejenga frem juu ya Mitaro ya kupitishia maji hivyo kufanya maji kutuhama.
Aidha, Kamati hiyo pia ilikagua usafi wa mazingira katika Viwanda na kuangalia mazingira ya ufanyaji kazi viwandani ambapo waliweza kutembelea kiwanda cha pasta, kiwanda cha madaftari pamoja na Kampuni ya uuzaji wa vifaa vya ujenzi (Kamaka Company Limited)
Kwa upande mwingine Kamati iliweza kiutembelea maeneo ya Dengu Beach kuona namna ambavyo bomba la maji ya mvua ambalo hutiririsha maji taka maeneo hayo ambapo kiasi cha shilingi millioni 4 kilitolewa kwaajili ya kufanya ukarabati kwa kuondoa mchanga ili bomba la maji ya mvua linalotiririsha maji taka maeneo ya Dengu beach kuelekezwa baharini.
Aidha Kamati imeridhia iundwe Kamati ndogo ya mazingira ambayo itakua inafanya ziara za kukagua mazingira kila mwezi kwani maeneo mengi viwandani hayaridhishi kabisa hivyo Kamati hiyo itakuwa ni moja ya mafanikio katika utunzaji wa mazingira na kupunguza athari za kimazingira kwa wananchi.
Naye, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Nyansika Motema akifanya majumuisho ya ziara hiyo amesema, "Leo tumetembelea baadhi ya miradi inayosimamiwa na kutekelezwa na Halmashauri ya Jiji la DSM ambapo tumeweza kuridhishwa na utekelezaji huo japo kuna marekebisho madogomadogo yakukamilisha hususani katika suala zima la utunzaji wa mazingira kwa baadhi yamaeneo ya viwandani na baadhi ya maeneo yanayotiririsha maji machafu yafanyiwe utekelezaji"
Sambamba na hilo Mhe. Nyansika ameendelea kusema, "Ziara yetu imekua na mafanikio makubwa kwani tumeweza kutembelea baadhi ya viwanda vinavyosimamiwa na Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam ambapo tumejionea Hali halisi ya mazingira jinsi yaliivyo katika viwanda vyetu kwani hali ya usafi hairidhishi kabisa hata hivyo sisi kama Kamati ya Mipango miji na Mazingira tunaelekeza viwanda vyote tulivyoviona haviko katika hali ya usafi kama kiwanda cha Madaftari (Five Stars) pamoja na Kamaka company Limited wachukuliwe hatua za kisheria kwakushindwa kutunza mazingira.”
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Anuani ya Posta: S.L.P 20950
Simu ya mezani: 0738 378 386
Namba ya Mkononi: 0738 378 386
Barua Pepe: info@dcc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.