Kamati ya Mipango Miji na Mazingira ya Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam chini ya Mwenyekiti wa Kamati wake Mhe. Nyansika Getama leo Agosti 13, 2024 wamefanya ziara ya ukaguzi wa miradi mbalimbali iliyotekelezwa kwa kipindi cha robo ya nne ya mwaka (Aprili - Juni 2024).
Miradi iliyotembelewa ni pamoja na bustani ya A to Z iliyopo Kata ya Kivukoni, Mradi jumuishi wa kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi katika Kata ya Vingunguti, Barabara ya Kitunda Machimbo (mita 600) pamoja na ukaguzi wa mfereji wa malapa.
Akiongea wakati wa majumuisho ya ziara hiyo, wajumbe wakiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Nyansika Getama wameishukuru Serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fungu kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ndani ya Jiji la Dar es Salaam na kukumbushana kutekeleza majukumu yao ipasavyo kwaajili ya kutatua changamoto za wananchi ambao wamewaweka wao madarakani.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Anuani ya Posta: S.L.P 20950
Simu ya mezani: 0738 378 386
Namba ya Mkononi: 0738 378 386
Barua Pepe: info@dcc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.