Na: Doina Mwambagi
Kamati ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Ilala, ikiongozwa na Mwenyekiti wake, Ndg. Said Sidde, imefanya ziara ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Jiji la Dar es Salaam leo, tarehe 19 Februari 2025. Ziara hii ni sehemu ya ufuatiliaji wa utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi.
Miradi iliyotembelewa inajumuisha ujenzi wa tanki la maji Bangulo lenye thamani ya Shilingi bilioni 36.8, ujenzi wa Shule ya ghorofa ya sekondari Amani yenye madarasa 20 na matundu 45 ya vyoo, mradi wenye thamani ya Shilingi bilioni 1.6, pamoja na ujenzi wa kituo cha afya cha ghoraofa cha Mchikichini chenye thamani ya Bilioni 2.7
Akiongea wakati wa ziara hiyo Mwenyekiti wa Kamati ya Siasa Ndg Said Sidde ameipongeza Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kwa kusimamia miradi hiyo kwa ufanisi, huku akibainisha kuwa thamani ya fedha inaonekana na miradi inatekelezwa kwa kiwango cha juu.
Akitoa taarifa ya maendeleo ya miradi hiyo kwa Kamati ya Siasa, Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Mhe. Edward Mpogolo, alisema ”Viongozi tuna deni kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa sababu fedha zote zilishatolewa. Hivyo ni matumaini yake kuona miradi yote katika sekta za elimu, afya, na barabara inakamilika kwa wakati.”
Aidha, Mkuu wa Wilaya alitoa wito kwa wasimamizi wa miradi kuhakikisha wanajituma na kufanya kazi kwa bidii ili miradi hiyo ikamilike kwa manufaa ya wananchi wa Ilala na maeneo ya jirani.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Anuani ya Posta: S.L.P 20950
Simu ya mezani: 0738 378 386
Namba ya Mkononi: 0738 378 386
Barua Pepe: info@dcc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.