Kamati ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Ilala yaridhishwa na matumizi ya fedha na kasi ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa kupitia fedha za mapato ya ndani ya Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam.
Hayo yameelezwa na Mwenyekiti CCM Wilaya ya Ilala Ndg. Said Sidde leo tarehe 18 Agostii, 2023 akiwa na Wajumbe wa Kamati ya Siasa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa miradi mbalimlbali ya maendeleo inayotekelezwa na Halmashauri ya Jiji la DSM.
Miradi iliyotembelewa na Kamati hiyo ni Ujenzi wa Madarasa matano (5) na Matundu sita (6) ya vyoo Shule ya Msingi Kombo, Ujenzi wa Shule mpya Mnyamani, Ujenzi wa Uwanja wa Michezo Shule ya Sekondari Benjamin Mkapa, Ukarabati wa Soko la Kariakoo pamoja na Ujenzi wq madarasa nane na Vyoo kumi na tatu (13) Shule ya Sekondari Jangwani.
Akihitimisha ziara hiyo Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ilala Ndg. Said Sidde amesema “Naipongeza sana Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kwa utekelezaji wa miradi kwani thamani ya fedha inaonekana pia miradi inatekelezwa kwa kiwango cha juu zaidi hii inaonyesha ni jinsi gani Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) inavyotekelezwa kwa kasi zaidi.”
Naye Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Edward Mpogolo amemuhakikishia Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Ilala kutekeleza yote aliyoyaagiza lengo likiwa ni Kutekeleza Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) pamoja na kusogeza huduma za kijamii karibuna Wananchi.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Anuani ya Posta: S.L.P 20950
Simu ya mezani: 0738 378 386
Namba ya Mkononi: 0738 378 386
Barua Pepe: info@dcc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.