• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Dar es Salaam City Council
Dar es Salaam City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Jiji
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Fedha, Utawala na Utumishi
      • Ujenzi na Zimamoto
      • Udhibiti Taka
      • Mipangomiji, Mazingira na Usafirishaji
      • Afya na Huduma za Tiba
    • Vitengo
      • Mipango, Ufuatiliaji na Takwimu
      • Sheria na Usalama
      • Itifaki, Uhusiano na Umma
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Ugavi na Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Shughuli za Utalii
      • Dar es Salaam Yetu
      • Misitu na Mashamba ya wanyama wafugwao
      • Sehemu za kitamaduni, ngoma za asili na sanaa za mikono
      • Kituo cha Urithi wa Ubunifu Majengo na Utalii
      • Maeneo ya kupumzika, bustani na viwanja vya michezo
      • Maeneo ya Manunuzi
      • Majengo na maeneo ya kihistoria
      • Uwanda wa bahari, fukwe na visiwa
    • Urejelezaji wa Taka Ngumu
  • Huduma Zetu
    • Vibali vya Pikipiki
    • Vibali vya Maegesho ya Teksi
    • Vibali vya Kuingiza Magari ya Mizigo
    • Vituo Vikuu vya Mabasi
    • Udhibiti Taka Ngumu
    • Taarifa za Historia ya Viwanja
    • Mazishi ya miili ya marehemu wasiokuwa na ndugu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha na Uongozi
      • Kamati ya Mipangomiji, Mazingira na Miundombinu
      • Kamati ya Mipango na Ufuatiliaji
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba ya Vikao vya Kisheria
    • Ratiba ya Mstahiki Meya
    • Mameya Wazamani wa Jiji
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi iliyo kwenye Mpango
    • Miradi Inayoendelea
    • Vitega Uchumi vya Jiji
  • Machapisho
    • Sheria
    • Sheria Ndogo
    • Sera
    • Miongozo
    • Taarifa mbalimbali
    • Fomu za Maombi
    • Fomu za Ahadi ya Uadilifu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Hotuba
    • Habari Mpya
    • Matukio

Kamati ya Siasa Wilaya ya Ilala yaridhishwa na utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Jiji la DSM

Tarehe iliyowekwa: August 15th, 2024

Kamati ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Ilala chini ya Mwenyekiti wake Ndg. Said Sidde leo tarehe 15 Agosti, 2024 imefanya ziara ukaguzi wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Jiji la DSM ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi.

Miradi iliyotembelewa na Kamati hiyo ni pamoja na Mradi wa Ujenzi wa ghorofa sita Shirika la Uchumi na Maendeleo la Jiji la DSM wenye thamani ya shilingi Bilioni 30, ujenzi wa Barabara ya Bima – Kimanga kiwango cha lami yenye urefu wa mita 400 wenye thamani ya milioni 593 ikiwa ni pamoja na ujenzi wa mitaro na kuweka taa za kisasa, Ujenzi wa vyumba vya madarasa 20 na matundu ya vyoo 45 katika Shule ya Sekondari Bonyokwa wenye thamani ya milioni 539.

Akiongea wakati wa ziara hiyo, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ilala Ndg. Said Sidde amesema “Naipongeza Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam wakiongozwa na Mstahiki Meya na Mkurugenzi, pia nampongeza Mkuu wa Wilaya ya Ilala kwa ongeze kubwa la mapato na kusimamia na kutekeleza miradi kwani thamani ya fedha inaonekana na miradi inatekelezwa kwa kiwango cha juu. Hii inaonyesha ni jinsi gani Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) inavyotekelezwa kwa kasi hivyo niwaombe kukamilisha miradi  ambayo bado inasuasua hasa barabara Bima - Kimanga kwani barabara hii ni muhimu kwa wakazi wa Tabata kwa usafirishaji.”

Pia, Ndg. Said Sidde ameongeza “Natoa maelekezo kwa viongozi na watendaji wa Halmshauri ya Jiji la DSM kuhakikisha mnachagua wakandarasi wazawa wenye uwezo na uzoefu ili waweze kukamilisha miradi kwa ubora na wakati ili wananchi waweze kufurahia huduma. Pia natoa wito kwa maeneo ya wazi yanayomilikiwa na Halmshauri mkaribishe wawekezaji wawekeze ili kuongeza ajira na mapato ya Halmashauri na Nchi kwa ujumla."

Awali akiwasilisha taarifa ya miradi na utekelezaji wa Ilani kwa Mwenyekiti wa CCM Wilaya pamoja na wajumbe wa Kamati ya Siasa Wilaya ya Ilala, Mkuu wa Wilaya ya hiyo Mhe. Edward Mpogolo ameeleza kuwa “Viongozi tuna deni kwa Rais wa Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania, kwa sababu fedha zote zilishatolewa. Hivyo ni matumaini yake kuona miradi yote katika sekta za Elimu, Afya, na Barabara inakamilika kwa wakati. Hivyo nitoe wito kwa wasimamizi wa miradi kujituma na kufanya kazi kwa bidii ili kukamilisha miradi kwa manufaa ya wananchi wa Ilala na maeneo ya jirani.”

Kwa upande Mstahiki Meya Mhe. Omary Kumbilamoto amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa pesa anazotoa kwa Halmashauri yetu, pia amemshukuru Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ilala kwa ziara aliyoifanya huku akimuhakikishia kutekeleza maelekezo yote aliyoyatoa kwa manufaa ya wananchi.

Matangazo

  • TAARIFA KWA UMMA February 19, 2025
  • TAARIFA KWA UMMA - MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA January 17, 2025
  • MATOKEO YA UPIMAJI WA KITAIFA WA DARASA LA NNE (SFNA) 2024 January 04, 2025
  • UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA, 2025 December 16, 2024
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • "Tutahakikisha tunasimamia Kata 36 na Mitaa 159 ili Jiji la DSM liwe safi" - DC Mpogolo

    May 03, 2025
  • Jiji La DSM laweka mikakati kushinda UMITASHUMTA ngazi ya Mkoa

    April 29, 2025
  • Wakazi wa Jiji la Dar es Salaam waadhimisha Muungano kwa kupanda miti na kufanya usafi wa mazingira

    April 26, 2025
  • Zoezi la usafi wa mwisho wa wiki laendelea

    April 12, 2025
  • Angalia zote

Video

Msimbazi Basin Development Project Implementation Area
Video Zingine

Viunganishi vya Haraka

  • Mameya wa zamani wa Jiji
  • Vibali vya kuingia na Pikipiki katikati ya Jiji
  • Udhibiti wa Taka ngumu Jijini
  • Eneo Maalum la Usafi Jijini
  • Kituo cha Urithi wa Ubunifu Majengo na Utalii
  • Uwanda wa Bahari, Fukwe na Visiwa
  • Sehemu za Kitamaduni, Ngoma za Asili na Sanaa za Mikono
  • Majengo na Maeneo ya Kihistoria
  • Maeneo ya Kupumzika, Bustani na Viwanja vya Michezo

Viunganishi Linganifu

  • BUNGE
  • Blogu ya Jiji
  • UTUMISHI
  • IKULU
  • TAMISEMI
  • IDARA YA HABARI MAELEZO

Wasomaji mbalimbali duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM

    Anuani ya Posta: S.L.P 20950

    Simu ya mezani: 0738 378 386

    Namba ya Mkononi: 0738 378 386

    Barua Pepe: info@dcc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.