Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dar es Salaam Bi. Kate Kamba leo tarehe 31 Mei, 2019 jijini Dar es Salaam akiwa na wajumbe wa Kamati ya Siasa ya CCM Mkoa wa Dar es Salaam wamefanya ziara katika Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kwa lengo la kukagua utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi kupitia miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Halmashauri ya Jiji.
Miradi iliyotembelewa na Kamati hiyo ni pamoja na ujenzi wa miundombinu katika eneo la kupumzikia DRIMP inayohusisha ukumbi wa nje wa maonyesho ya kiutamaduni, ukumbi wa ndani wa mikutano pamoja na ujenzi wa maduka 19 ya biashara.
Wajumbe wa Kamati ya Siasa ya Mkoa pia walitembelea mradi wa ujenzi wa viwanda vidogo vidogo katika eneo la Mwananyamala ambao unahusisha ujenzi wa viwanda vidogo vidogo 6, choo cha umma matundu 10, mgahawa na maduka ya biashara 7.
Kamati pia ilitembelea na kujionea utekelezaji wa Mradi wa Kimkakati wa ujenzi wa Kituo Kikuu cha Mabasi katika eneo la Mbezi Luis unaokadiriwa kugharimu kiasi cha jumla ya Shilingi 50,947,589,580.20 bila kodi ya zuio "VAT Exclusive" fedha kutoka Serikali Kuu.
Akizungumza wakati wa majumuisho ya ziara hiyo kwa wajumbe wa Kamati ya Siasa na baadhi ya watumishi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, Bi. Kate Kamba alitoa pongezi kwa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam na kuwasihi wawe wabunifu katika kuanzisha vyanzo vipya vya mapato ili kuweza kufikia lengo la utoaji huduma bora kwa wananchi wa Dar es Salaam na Watanzania wote kwa ujumla.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Anuani ya Posta: S.L.P 20950
Simu ya mezani: 0738 378 386
Namba ya Mkononi: 0738 378 386
Barua Pepe: info@dcc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.