• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Dar es Salaam City Council
Dar es Salaam City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Jiji
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Fedha, Utawala na Utumishi
      • Ujenzi na Zimamoto
      • Udhibiti Taka
      • Mipangomiji, Mazingira na Usafirishaji
      • Afya na Huduma za Tiba
    • Vitengo
      • Mipango, Ufuatiliaji na Takwimu
      • Sheria na Usalama
      • Itifaki, Uhusiano na Umma
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Ugavi na Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Shughuli za Utalii
      • Dar es Salaam Yetu
      • Misitu na Mashamba ya wanyama wafugwao
      • Sehemu za kitamaduni, ngoma za asili na sanaa za mikono
      • Kituo cha Urithi wa Ubunifu Majengo na Utalii
      • Maeneo ya kupumzika, bustani na viwanja vya michezo
      • Maeneo ya Manunuzi
      • Majengo na maeneo ya kihistoria
      • Uwanda wa bahari, fukwe na visiwa
    • Urejelezaji wa Taka Ngumu
  • Huduma Zetu
    • Vibali vya Pikipiki
    • Vibali vya Maegesho ya Teksi
    • Vibali vya Kuingiza Magari ya Mizigo
    • Vituo Vikuu vya Mabasi
    • Udhibiti Taka Ngumu
    • Taarifa za Historia ya Viwanja
    • Mazishi ya miili ya marehemu wasiokuwa na ndugu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha na Uongozi
      • Kamati ya Mipangomiji, Mazingira na Miundombinu
      • Kamati ya Mipango na Ufuatiliaji
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba ya Vikao vya Kisheria
    • Ratiba ya Mstahiki Meya
    • Mameya Wazamani wa Jiji
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi iliyo kwenye Mpango
    • Miradi Inayoendelea
    • Vitega Uchumi vya Jiji
  • Machapisho
    • Sheria
    • Sheria Ndogo
    • Sera
    • Miongozo
    • Taarifa mbalimbali
    • Fomu za Maombi
    • Fomu za Ahadi ya Uadilifu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Hotuba
    • Habari Mpya
    • Matukio

Kamati ya Uchumi na Huduma za Jamii Jiji la DSM yafanya Ziara ya ukaguzi wa Miradi ya Afya

Tarehe iliyowekwa: April 30th, 2024

Kamati ya Uchumi na Huduma za Jamii Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam leo Aprili 30, 2024 imefanya ziara ya ukaguzi wa Miradi ya Afya lengo likiwa ni kufuatilia utekelezaji wa shughuli za kimaendeleo zilizotekelezwa na Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kwa kipindi cha robo ya tatu kwa mwaka wa fedha 2023/2024 kilichoanza Januari hadi Machi 2024.

Ziara hiyo ililenga kutembelea na kukagua miradi mbalimbali ya Afya inayoendelea kutekelezwa na Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kujionea maendeleo ya miradi hiyo jinsi  itakavyorahisisha huduma mbalimabali za afya kwa Jamii pindi itakapokamilika.

Aidha, Miradi iliyotembelewa ni pamoja na ujenzi wa jengo la kuhifadhia maiti katika Kituo cha Afya Chanika uliogharimu kiasi cha shilingi milioni 107 ujenzi ukiwa katika hatua ya umaliziaji, ujenzi wa jengo la mionzi (X-Ray) Kituo cha Afya Pugu uliogharimu kiasi cha shilingi milioni 107 utekelezaji wa mradi ukiwa hatua ya ukamilishaji pamoja na uwekaji mashine ya mionzi huku ujenzi wa ghorofa 5 Kituo cha Afya Mchikichini ukiwa umekamilika kwa asilimia 40 ambapo sakafu mbili zimekamilika na sakafu ya tatu imeanza kujengwa.

Akizungumza katika ziara hiyo Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mheshimiwa Saady Khimji amesema kuwa “Leo tumetembelea baadhi ya Miradi ya Afya inayosimamiwa na kutekelezwa na Halmashauri ya Jiji la DSM ambapo tumeweza kuridhishwa na utekelezaji huo hivyo nitoe wito kwa Watendaji wa Halmashauri kusimamia miradi hii kwa ukaribu zaidi na Sisi kama wasimamizi tutaendelea kushirikiana nao kuhakikisha miradi hii inatekelezwa kwa wakati na thamani ya Fedha inayotumika inalingana na ubora wa miradi kwani Kamati hufanya ziara hizi kwa lengo la kukagua na kuhakikisha fedha zinazotolewa na Serikali Kuu pamoja na Halmashauri zinawafikia walengwa na kufanya kazi kama ambavyo fedha hizo zimeelekeza.  Hivyo naomba mapungufu yaliyoonekana kwenye miradi hii yashughulikiwe kwa wakati ili wananchi wote wafikiwe na huduma muhimu na bora kwa wakati kama Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anavyoonesha juhudi zake katika kuwahudumia Wananchi.”

Sambamba na hilo Mhe. Khimji ameendelea kusema ni wajibu wa kila Mtendaji kuhakikisha anasimamia vyema shughuli za maendeleo ili kuunga mkono jitihada za Serikali katika kuleta maendeleo ya pamoja kwa Jamii

“Sera ya Serikali ni kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora na kwa wakati kwani sisi kama wasimamizi hatutavumilia watu wanaokwamisha kwa makusudi miradi ya maendeleo hivyo nipende kutoa wito kwa Mkurugenzi wa Jiji la Dar es salaam kuhakikisha anashirikiana na watendaji wake kwa ukaribu kusimamia miradi hii ya afya ikamilike kwa wakati uliopangwa lengo ni kuwasaidia wananchi wetu kupata huduma bora kwa wakati. Pia tusisahau kuwashirikisha wananchi katika kufanikisha miradi kwani miradi hii inawalenga wao moja kwa moja." Amesisitiza Mhe. Khimji.

Aidha, Wajumbe wa Kamati wameridhia kuwa endapo kutakua na changamoto wakati wa utekelezaji wa miradi ni vyema changamoto hizo zikawasilishwa sehemu husika mapema na kufanyiwa kazi ili maendeleo ya wananchi yasikwamishwe huku wakiagiza wahandisi kutoka Halmashauri kuhakikisha wanasimamia kwa ukaribu zaidi ujenzi wa Miradi ya Maendeleo ili miradi hiyo ikamilike kwa wakati na iwe yenye ubora.

Matangazo

  • TAARIFA KWA UMMA February 19, 2025
  • TAARIFA KWA UMMA - MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA January 17, 2025
  • MATOKEO YA UPIMAJI WA KITAIFA WA DARASA LA NNE (SFNA) 2024 January 04, 2025
  • UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA, 2025 December 16, 2024
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • "Tutahakikisha tunasimamia Kata 36 na Mitaa 159 ili Jiji la DSM liwe safi" - DC Mpogolo

    May 03, 2025
  • Jiji La DSM laweka mikakati kushinda UMITASHUMTA ngazi ya Mkoa

    April 29, 2025
  • Wakazi wa Jiji la Dar es Salaam waadhimisha Muungano kwa kupanda miti na kufanya usafi wa mazingira

    April 26, 2025
  • Zoezi la usafi wa mwisho wa wiki laendelea

    April 12, 2025
  • Angalia zote

Video

Msimbazi Basin Development Project Implementation Area
Video Zingine

Viunganishi vya Haraka

  • Mameya wa zamani wa Jiji
  • Vibali vya kuingia na Pikipiki katikati ya Jiji
  • Udhibiti wa Taka ngumu Jijini
  • Eneo Maalum la Usafi Jijini
  • Kituo cha Urithi wa Ubunifu Majengo na Utalii
  • Uwanda wa Bahari, Fukwe na Visiwa
  • Sehemu za Kitamaduni, Ngoma za Asili na Sanaa za Mikono
  • Majengo na Maeneo ya Kihistoria
  • Maeneo ya Kupumzika, Bustani na Viwanja vya Michezo

Viunganishi Linganifu

  • BUNGE
  • Blogu ya Jiji
  • UTUMISHI
  • IKULU
  • TAMISEMI
  • IDARA YA HABARI MAELEZO

Wasomaji mbalimbali duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM

    Anuani ya Posta: S.L.P 20950

    Simu ya mezani: 0738 378 386

    Namba ya Mkononi: 0738 378 386

    Barua Pepe: info@dcc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.