• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Dar es Salaam City Council
Dar es Salaam City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Jiji
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Fedha, Utawala na Utumishi
      • Ujenzi na Zimamoto
      • Udhibiti Taka
      • Mipangomiji, Mazingira na Usafirishaji
      • Afya na Huduma za Tiba
    • Vitengo
      • Mipango, Ufuatiliaji na Takwimu
      • Sheria na Usalama
      • Itifaki, Uhusiano na Umma
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Ugavi na Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Shughuli za Utalii
      • Dar es Salaam Yetu
      • Misitu na Mashamba ya wanyama wafugwao
      • Sehemu za kitamaduni, ngoma za asili na sanaa za mikono
      • Kituo cha Urithi wa Ubunifu Majengo na Utalii
      • Maeneo ya kupumzika, bustani na viwanja vya michezo
      • Maeneo ya Manunuzi
      • Majengo na maeneo ya kihistoria
      • Uwanda wa bahari, fukwe na visiwa
    • Urejelezaji wa Taka Ngumu
  • Huduma Zetu
    • Vibali vya Pikipiki
    • Vibali vya Maegesho ya Teksi
    • Vibali vya Kuingiza Magari ya Mizigo
    • Vituo Vikuu vya Mabasi
    • Udhibiti Taka Ngumu
    • Taarifa za Historia ya Viwanja
    • Mazishi ya miili ya marehemu wasiokuwa na ndugu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha na Uongozi
      • Kamati ya Mipangomiji, Mazingira na Miundombinu
      • Kamati ya Mipango na Ufuatiliaji
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba ya Vikao vya Kisheria
    • Ratiba ya Mstahiki Meya
    • Mameya Wazamani wa Jiji
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi iliyo kwenye Mpango
    • Miradi Inayoendelea
    • Vitega Uchumi vya Jiji
  • Machapisho
    • Sheria
    • Sheria Ndogo
    • Sera
    • Miongozo
    • Taarifa mbalimbali
    • Fomu za Maombi
    • Fomu za Ahadi ya Uadilifu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Hotuba
    • Habari Mpya
    • Matukio

Kamati ya Ustawi wa Jamii Zanzibar yafanya ziara ya mafunzo Jiji la DSM

Tarehe iliyowekwa: November 8th, 2022

Kamati ya Ustawi wa Jamii kutoka Visiwani Zanzibar leo tarehe 8 Novemba, 2022 imefanya ziara katika Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kuja kubadilishana uzoefu katika Idara ya Elimu Maalumu katika Jiji la Dar es Salaam ambapo msafara huo uliongozwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Malindi Mhe. Mohamedi Ahmada Salum pia Mbunge na Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe. Ally Abdul-Ghulam Hussein.

Wakiwa katika viunga vya Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam walipokelewa na Kaimu Mkurugenzi wa JIji la Dar es Salaam Eng. Amani Mafuru na kuweza kubadilishana uzoefu  Kaimu Mkurugenzi wa Jiji anasema “Nachukua nafasi hii kuwakaribisha katika Jiji la Dar es Salaam na tumefarijika kupokea ugeni huu Mkubwa kutoka Zanzibar, hii inatupa uwezo wa kubadilishana uzoefu jinsi ya kuendesha shule maalumu”.

Sambamba na hilo ugeni huo uliweza kutembelea Shule ya Msingi Uhuru Mchanganyiko iliyopo katika Halmshauri ya Jiji la Dar es Salaam kujifunza na kujionea shughuli za kielimu zinazofanyika katika shule hiyo, shule kongwe ya Msingi Uhuru Mchanganyiko ambayo inachukua wanafunzi mbalimbali wenye ulemavu tofauti ikiwa ni pamoja na wanafunzi wasioona, viziwi wasioona, wanafunzi wenye ulemavu wa akili na ulemavu wa ngozi.

Pia, Ugeni huo ulipata fursa ya kutembelea Shule ya Msingi Buguruni Viziwi ambayo ni maalumu kwa kufundisha wanafunzi wasiosikia ili kuwawezesha kufanya mawasiliano ya kila siku pamoja na kupata elimu, mafanikio katika ufundishaji wa shule hiyo umeenda katika mapana makubwa, akiongea  Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Buguruni viziwi Bw. Yahaya Maftaa anasema

“Shule ya Msingi Buguruni viziwi imefikia mafanikio makubwa kwani wanafunzi wanaoanzia ngazi ya awali mpaka darasa la saba wanakuja hapa hawajui lolote lakini wanatoka hapa wanajua kusoma na kuandika na kuwasiliana kwa lugha za alama pia mpaka sasa tuna wanafunzi watatu ambao wamefika Chuo Kikuu Kutoka hapa”.

Mwenyekiti wa Kamati ya Ustawi wa Jamii kutoka Visiwani Zanzibar Mhe. Mohamedi Salumu amesisitiza na kuipongeza Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kwa watendaji wote, walimu, maafisa Elimu kitengo Maalumu kwa kuweza kufanikisha na kuwalea wanafunzi wote wenye mahitaji maalumu tumejifunza vitu vingi sana katika Shule hii ya Uhuru Mchanganyiko pamoja na Buguruni Viziwi kupitia ziara hii. “Kwa hakika sisi kama kamati kwa niaba ya wote tunaishukuru sana Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kwa ziara hii tumejifunza vya kutosha na tunaimani tumebadilishana uzoefu vya kutosha na kuweza kuyafanyia kazi tukirudi Zanzibar pia Nachukua nafasi hii kuipongeza Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kuwawezesha watoto hawa kupata elimu stahiki”

Naye Mjumbe wa kamati ya Ustawi wa Jamii ambaye pia ni Mbunge na Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe. Abdul-Ghulan Hussein amesema

“Lengo letu ni kuja kujionea shule hizi zinavyoendeshwa na kubdilishana uzoefu ili sisi situweze kuendesha na kuzidisha ufanisi kupitia ziara hii pia tunaweza kupata fursa sisi kama Wizara kutuma kamati kuja kujifunza zaidi na kuimarisha ushirikiano”

Matangazo

  • Matokeo ya upimaji wa Kitaifa wa Darasa la Nne 2022 January 04, 2023
  • Matokeo ya upimaji wa Kitaifa wa Kidato cha Pili 2022 January 04, 2023
  • Taarifa kwa Umma kuhusu Wanafunzi kuripoti shuleni mwaka 2023 January 12, 2023
  • TANGAZO DHIDI YA UTAPELI WA AJIRA July 20, 2022
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • Katibu Tawala Wilaya ya Ilala aongoza zoezi la usafi wa mwisho wa mwezi

    January 28, 2023
  • Naibu Meya Jiji la DSM azindua jengo la Ofisi ya Kata ya Mzinga

    January 27, 2023
  • Bodi ya Afya ya Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam yawataka wakandarasi kukamilisha mifumo ya umeme na maji kwa wakati

    January 26, 2023
  • Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Ilala yaipongeza Idara ya Maendeleo ya Jamii kwa kuweka mikakati mizuri ya kulinda haki za Watoto

    January 23, 2023
  • Angalia zote

Video

NAPA
Video Zingine

Viunganishi vya Haraka

  • Mameya wa zamani wa Jiji
  • Vibali vya kuingia na Pikipiki katikati ya Jiji
  • Udhibiti wa Taka ngumu Jijini
  • Eneo Maalum la Usafi Jijini
  • Kituo cha Urithi wa Ubunifu Majengo na Utalii
  • Uwanda wa Bahari, Fukwe na Visiwa
  • Sehemu za Kitamaduni, Ngoma za Asili na Sanaa za Mikono
  • Majengo na Maeneo ya Kihistoria
  • Maeneo ya Kupumzika, Bustani na Viwanja vya Michezo

Viunganishi Linganifu

  • BUNGE
  • Blogu ya Jiji
  • UTUMISHI
  • IKULU
  • TAMISEMI
  • IDARA YA HABARI MAELEZO

Wasomaji mbalimbali duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM

    Anuani ya Posta: S.L.P 20950

    Simu ya mezani: 2128800

    Namba ya Mkononi: 0713614364

    Barua Pepe: info@dcc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.