Diwani wa Kata ya Kinyerezi Mhe. Leah Mgitu amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuipa kipaumbele sekta ya Elimu nchini ikiwemo kata yake ya Kinyerezi.
Mhe. Mgitu ameyasema hayo alipokuwa akipokea madawati 300 yaliyotolewa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam katika kata ya Kinyerezi na kugawiwa katika shule za Kibaga, Zimbili pamoja na Kinyerezi Jaika.
"Namshukuru Mhe. Rais kwa kuendelea kuipigania sekta ya Elimu katika kata yetu ya Kinyerezi, pia namshukuru Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kwa ajili ya kutupatia madawati haya ambayo yametokana na mapato ya ndani ya Halmashauri." mesema Mgitu
Aidha, amewashukuru viongozi wote wa Chama na Serikali wakiongozwa na Mbunge wa Jimbo la Segerea Mhe. Bonnah Kamoli kwa kuendelea kufanya kazi kwa bidii katika kuhakikisha wanatekeleza vyema Ilani ya Chama Cha Mapinduzi.
Naye Juma Swai ambaye ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi tawi la Zimbili amemshukuru Mhe. Dkt .Samia Suluhu Hassan, Mbunge wa Jimbo la Segerea, Diwani wa Kata ya Kinyerezi kwa kuendelea kuwafikia wananchi na kutatua kero zao mbalimbali kwani ndicho wanachokihitaji kutoka kwao.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Anuani ya Posta: S.L.P 20950
Simu ya mezani: 0738 378 386
Namba ya Mkononi: 0738 378 386
Barua Pepe: info@dcc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.