• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Dar es Salaam City Council
Dar es Salaam City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Jiji
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Fedha, Utawala na Utumishi
      • Ujenzi na Zimamoto
      • Udhibiti Taka
      • Mipangomiji, Mazingira na Usafirishaji
      • Afya na Huduma za Tiba
    • Vitengo
      • Mipango, Ufuatiliaji na Takwimu
      • Sheria na Usalama
      • Itifaki, Uhusiano na Umma
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Ugavi na Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Shughuli za Utalii
      • Dar es Salaam Yetu
      • Misitu na Mashamba ya wanyama wafugwao
      • Sehemu za kitamaduni, ngoma za asili na sanaa za mikono
      • Kituo cha Urithi wa Ubunifu Majengo na Utalii
      • Maeneo ya kupumzika, bustani na viwanja vya michezo
      • Maeneo ya Manunuzi
      • Majengo na maeneo ya kihistoria
      • Uwanda wa bahari, fukwe na visiwa
    • Urejelezaji wa Taka Ngumu
  • Huduma Zetu
    • Vibali vya Pikipiki
    • Vibali vya Maegesho ya Teksi
    • Vibali vya Kuingiza Magari ya Mizigo
    • Vituo Vikuu vya Mabasi
    • Udhibiti Taka Ngumu
    • Taarifa za Historia ya Viwanja
    • Mazishi ya miili ya marehemu wasiokuwa na ndugu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha na Uongozi
      • Kamati ya Mipangomiji, Mazingira na Miundombinu
      • Kamati ya Mipango na Ufuatiliaji
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba ya Vikao vya Kisheria
    • Ratiba ya Mstahiki Meya
    • Mameya Wazamani wa Jiji
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi iliyo kwenye Mpango
    • Miradi Inayoendelea
    • Vitega Uchumi vya Jiji
  • Machapisho
    • Sheria
    • Sheria Ndogo
    • Sera
    • Miongozo
    • Taarifa mbalimbali
    • Fomu za Maombi
    • Fomu za Ahadi ya Uadilifu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Hotuba
    • Habari Mpya
    • Matukio

Maafisa Ustawi wahimizwa kutoa Elimu kwa jamii juu ya maswala ya Ukatili wa kijinsia

Tarehe iliyowekwa: August 6th, 2024

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Albert Chalamila amewahimiza maafisa ustawi kuhakikisha wanatoa elimu kwa Jamii juu ya masuala ya ukatili wa kijinsia na kuhakikisha wanakemea vitendo hivyo, hayo ameyabainisha Leo Agosti 6,2024 wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Maafisa Ustawi wa Jamii Mkoa unaofanyika katika Ukumbi wa Karimjee Jijini Dar es Salaam ambao unatarajiwa kuhitimishwa Agosti 7, 2024 lengo likiwa ni kutoa fursa kwa Maafisa Ustawi wa Jamii kubadilishana uzoefu, kujifunza na kuunda mtandao wa ushirikiano ambao utasaidia katika kuboresha huduma za kijamii nchini pamoja na kukemea vikali vitendo vya  ukatili wa kijinsia na taharuki za utekaji zisizo za kweli zinazoendelea kwenye jamii.

Akizungumza wakati wa ufunguzi huo, Mhe. Chalamila ameeleza kuwa Sekta ya Ustawi wa Jamii ni sekta muhimu sana kwa Jamii kwani inamuhusu mwananchi moja kwa moja hivyo kutokana na umuhimu wa sekta hiyo kumesababisha kuanzishwa kwa vyombo vya habari kwakua dunia ya sasa mambo mengi yanayoendelea huonekana sana mtandaoni hivyo, vyombo hivi vya habari vitakuwa ni chanzo cha kufikisha taarifa na elimu kuhusu ustawi wa jamii kwa wakati husika.

Sambamba na hilo, Mhe. Chalamaila amezindua channel maalum ya mtandaoni ya ustawi wa jamii iitwayo "Ustawi wa Jamii Dsm Digital" iliyoambatana na kukabidhi vifaa vya kuchakata habari ikiwemo kompyuta mpakato (laptop), kamera na vifaa vingine vitakavyotumiwa na vitengo vya ustawi wa jamii katika Halmashauri za Manispaa zote za Mkoa wa Dar es Salaam.

Halikadhalika, Mhe. Chalamila amewataka Maafisa Ustawi wa Jamii kufanya kazi kwa bidii na weledi mkubwa ili kuhakikisha huduma bora zinawafikia wananchi wote huku akisisitiza kuwa Serikali itaendelea kutoa ushirikiano na rasilimali muhimu kwa maafisa hao ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi.

Aidha, Mhe. Chalamila alikabidhiwa tuzo ya kutambua mchango wake katika ustawi wa jamii na kupata fursa ya kutoa tuzo kwa Katibu Tawala wa Mkoa Dkt. Toba Nguvila, Mganga Mkuu wa Mkoa Dkt. Mohammed Mang'una pamoja na viongozi wengine kwa kutambua mchango wao katika sekta hiyo.

Awali Akiongea kwa Niaba ya Wakurugenzi wote wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Tabu Faith Shaibu amewahimiza Maafisa Ustawi wote wa Mkoa kuhakikisha wanatumia vizuri fursa hiyo ya vyombo vya habari kwani vyombo vya habari ni muhimili muhimu sana katika kuhabarisha Umma.

“Hatua hii ni muhimu sana kwa kutambua vyombo vya Habari kwani kupitia vyombo hivi naamini watu watapata elimu ya kutosha na sisi tutao ushirikiano wetu kuhakikisha jambo hili linafanikiwa katika Mkoa wa Dar es Salaam pia niwasihi Maafisa Ustawi wa Jamii  kutumia fursa hii kwani vyombo vya habari ni muhimili mkubwa wa kutoa taarifa kwa umma hivyo tuvipe kipaumbele ili tuweze kufikia lengo hivyo tunatoa Shukrani zetu kwa Mkuu wa Mkoa kutuzindulia vyombo hivi hivyo tupo tayari kupokea maelekezo yako ili kuleta ufanisi katika Mkoa wetu wa Dar es Salaam”. Amesema Bi. Shaibu.



Matangazo

  • TAARIFA KWA UMMA February 19, 2025
  • TAARIFA KWA UMMA - MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA January 17, 2025
  • MATOKEO YA UPIMAJI WA KITAIFA WA DARASA LA NNE (SFNA) 2024 January 04, 2025
  • UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA, 2025 December 16, 2024
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • "Tutahakikisha tunasimamia Kata 36 na Mitaa 159 ili Jiji la DSM liwe safi" - DC Mpogolo

    May 03, 2025
  • Jiji La DSM laweka mikakati kushinda UMITASHUMTA ngazi ya Mkoa

    April 29, 2025
  • Wakazi wa Jiji la Dar es Salaam waadhimisha Muungano kwa kupanda miti na kufanya usafi wa mazingira

    April 26, 2025
  • Zoezi la usafi wa mwisho wa wiki laendelea

    April 12, 2025
  • Angalia zote

Video

Msimbazi Basin Development Project Implementation Area
Video Zingine

Viunganishi vya Haraka

  • Mameya wa zamani wa Jiji
  • Vibali vya kuingia na Pikipiki katikati ya Jiji
  • Udhibiti wa Taka ngumu Jijini
  • Eneo Maalum la Usafi Jijini
  • Kituo cha Urithi wa Ubunifu Majengo na Utalii
  • Uwanda wa Bahari, Fukwe na Visiwa
  • Sehemu za Kitamaduni, Ngoma za Asili na Sanaa za Mikono
  • Majengo na Maeneo ya Kihistoria
  • Maeneo ya Kupumzika, Bustani na Viwanja vya Michezo

Viunganishi Linganifu

  • BUNGE
  • Blogu ya Jiji
  • UTUMISHI
  • IKULU
  • TAMISEMI
  • IDARA YA HABARI MAELEZO

Wasomaji mbalimbali duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM

    Anuani ya Posta: S.L.P 20950

    Simu ya mezani: 0738 378 386

    Namba ya Mkononi: 0738 378 386

    Barua Pepe: info@dcc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.