Zaidi ya shilingi Tsh. Bilioni 50 zimeletwa na Serikali ya Awamu ya Sita katika Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kwaajili ya kuboresha Sekta ya elimu ikiwemo elimu ya awali, Msingi na Sekondari ambapo fedha hizo zimetumika katika ujenzi wa miundombinu na ununuzi wa vifaa Mashuleni.
Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Ndg. Jomaary Satura leo Novemba 04, 2023 wakati wa mkutano wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam na vyombo vya habari kwa kushirikiana na Idara ya Habari Maelezo kwenye kampeni ya kutangaza mafanikio ya awamu ya sita chini ya Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kipindi cha miaka mitatu kwa Mikoa na Halmashauri iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Yombo 4 Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Akitoa shukrani kwa Serikali ya awamu ya sita kwa niaba ya Wananchi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Ndg. Satura amesema “Kwa kuona umuhimu wa Elimu kwa Wananchi wa Jiji la Dar es Salaam Serikali ya Awamu ya sita imeweza kuleta takribani shilingi billion 50 kwa ajili kuboresha sekta ya elimu kwa kujenga vyumba vya madarasa, uboreshaji wa miundombinu ya elimu pamoja na ununuzi wa vifaa mashuleni ambapo mwaka 2021 tulikua tunauwezo wa kuchukua wanafunzi elfu 24 kwenda Sekondari lakini kutokana na Jitihada za Rais Dkt Samia Suluhu Hassan za kuboresha huduma za elimu tumeweza kuongeza wanafunzi hadi kufika elfu 32 na wanafunzi hao wanahudhuria masomi hii inaonesha jitihada za Mheshimiwa Rais katika kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora na kwa Wakati”. Ameyasema Ndg. Satura.
Akiendelea kuwasilisha taarifa hiyo Ndg. Satura amesema “Kwa kipindi cha miaka mitatu Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kupitia asilimia 10% ya mapato yake ya ndani imewezesha takribani shilingi bilioni 17 kwa ajili ya mikopo ya vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye ulemavu na kufanya kufanya jumla ya mikopo tuliyotoa kufikia shilingi bilioni 27 ambazo zimepelekwa kwa vikundi takribani 880 na kuzalisha ajira kwa vijana pamoja na kuunga Mkono Juhudi za Mheshimiwa Rais za kukuza uchumi ambapo kwa Mwaka wa fedha 2023/2024 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam inatarajia kupeleka zaidi ya bilioni 8 mpaka 9 kwaajili ya kuwezesha Makundi maalumu.”
Sambamba na hilo Ndg. Satura amesema kutokana na mikopo hiyo Halmashauri imeweza kutengeneza viwanda zaidi ya 30 ambapo katika hivyo kiwanda cha walemavu cha Dege kinachotengeneza vifaa mbalimbali vya chuma ikiwemo vitanda pamoja na vithibiti mwendo (wheel Chairs) kimeweza kufanya kazi kwa ubora zaidi hadi kupelekea walemavu kutoonekana wawakizurura mjini kwakua wamepata ajira huku vijana wakiwezesha kwa kupatiwa bajaji zaidi ya 546 zenye thamani ya shilingi bilioni 1.3 pamoja na vijana walemavu bajaji 211 na bodaboda 546.
Aidha Ndg.Satura ameendelea kusema kuwa “Halmashauri yetu sasa katika jitihada za kumuunga mkono Mhe. Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassani kulipa ya Jiji la Dar es Salaam kuwa kutibu cha kiuchumi tumeweza kutenga takribani Bilioni 100 kwa ajili ya ujenzi wa masoko makubwa ya Mchikichini, Ilala, Gongolamboto na Chanika lakini pia tumeweza kutenga fedha shilingi bilioni 15 kwaajili ya kuongeza bajeti ya kuboresha elimu huku bilioni 25 zikitengwa kwaajili ya kuongeza bajeti ya afya katika Jiji letu hii ikiwa ni mikakati ya kurahisisha upatikanaji wa huduma muhimu katika Jiji letu.”
Kampeni ya kutangaza mafanikio ya Serikali ya awamu ya sita chini ya kauli mbiu “Tumekusikia Tumekufikia” imehudhuriwa na Msemaji Mkuu wa Serikali Ndg. Mobhare Matinyi, Mhe. Albert Chalamila Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam pamoja na Wakurugenzi wa Halmashauri za Mkoa wa Dar es Salaam.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Anuani ya Posta: S.L.P 20950
Simu ya mezani: 0738 378 386
Namba ya Mkononi: 0738 378 386
Barua Pepe: info@dcc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.