Watendaji mbalimbali wa sekta ya afya wa majiji ya Hamburg la Ujerumani na Dar es Salaam Tanzania jana wakutana kujadili namna bora ya kuhakikisha watu wa kipato cha chini wanapata huduma bora za afya.
Mkutano huo wa siku mbili ni sehemu ya ushirikiano kati ya majiji hayo mawili ulioanza tangu mwaka 2010 ukilenga kushirikiana katika nyanja mbalimbali za maendeleo.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano huo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa taasisi ya Christian Social Services Commission (CSSC) Peter Maduki alisema unatokana na jitihada za watu wa Jiji la Hamburg kwa kushirikiana na makanisa ya Tanzania kupitia CSSC wenye lengo la kuhakikisha watu wasio na uwezo wanapata huduma za afya.
“Jitihada hizi za pamoja zilianza mwezi Februari 2013 kwa majadiliano yaliyofuatiwa na mkutano uliofanyika jijini Hamburg mwezi Septemba 2013 ambao ulihudhuriwa na wawakilishi wa makanisa, asasi zisizo za kiserikali, na wawakilishi wa serikali kutoka Wizara ya Afya pamoja na Jiji la Dar es Salaam,” alieleza.
Katika mkutano huo walikubaliana kushirikiana, kubadilishana uzoefu kwenye masuala ya afya ya jamii pamoja, kuzuia magonjwa, kuweka mikakati ya kuboresha huduma za afya pamoja na kutoa kipaumbele cha ushirikiano kati ya sekta binafsi na umma “Public Private Partnership”.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Anuani ya Posta: S.L.P 20950
Simu ya mezani: 0738 378 386
Namba ya Mkononi: 0738 378 386
Barua Pepe: info@dcc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.