Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, Bi. Sipora Liana amefunga mafunzo ya watoa huduma ya usafiri pamoja na huduma ya chakula kwa watalii katika Chuo cha Utalii cha Taifa Dar es Salaam. Mafunzo hayo yaliyohusisha madereva Taxi 25 na Mama Lishe 25 yalianza tarehe 9/04/2018 na kumalizika tarehe 14/04/2018, ambayo yametolewa na Chuo cha Utalii cha Taifa chini ya ufadhili wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam.
Aidha, Mkurugenzi amewapongeza sana kwa kumaliza mafunzo yao salama na amewataka madereva na mama lishe hao kuendelea kujiendeleza na kuyafanyia kazi yale waliyofundishwa na kutoa elimu kwa wengine ili tuweze kufikia malengo ya kuendeleza na kukuza utalii katika Jiji la Dar es Salaam.
Hivi karibuni Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam ilizindua mpango wa kukuza na kuendeleza utalii ili kuhakikisha vivutio vingi vya utalii vinavyohusu historia ya nchi hii, mila, desturi na utamaduni, majengo ya kihistoria, siasa, uchumi na mambo ya jamii vinatangazwa ili kukuza utalii katika Jiji la Dar es Salaam na kuweza kutunza mazingira, kutoa ajira kwa wananchi wetu na pia kuchangia pato la Taifa.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Anuani ya Posta: S.L.P 20950
Simu ya mezani: 0738 378 386
Namba ya Mkononi: 0738 378 386
Barua Pepe: info@dcc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.