Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita leo tarehe 16 Agosti, 2018 amekutana na kufanya mazungumzo na ujumbe wa viongozi 20 wakiongozwa na Waziri wa Mamlaka ya Jiji la Kampala Bi. Benny Namugwanya Bugembe kutoka nchini Uganda ambapo pamoja na mambo mengine wamezungumzia suala la ukuaji wa maendeleo ya majiji barani Afrika.
Katika mazungumzo hayo, Meya Mwita ametumia nafasi hiyo kueleza mafanikio ya Jiji la Dar es Salaam katika sekta ya usafiri na usafirishaji hususani ujenzi wa miundombinu ya mabasi yaendayo haraka, reli ya kisasa pamoja jitihada za Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam katika kukuza na kuendeleza utalii jijini Dar es Salaam.
Kwaupande wake Waziri wa Jiji la Kampala kutoka Ofisi ya Rais, Bi. Benny Namugwanya Bugembe, amesema kuwa amefurahishwa na mazingira mazuri ya Jiji la Dar es Salaam na ziara yao imekuwa ni elimu tosha kwani wamepata fursa ya kubadilishana ujuzi na uzoefu katika kwa lengo la kuwaletea maendeleo wananchi.
Amefafanua kuwa,”maendelo katika nchi yoyote hutokana na kujifunza kwa jirani, tumeona mazingira mazuri, tunachukua na kupeleka kwetu, tunakupongeza Meya kwa kuleta maendeleo kwenye Jiji lako” amesema Waziri Benny.
Ugeni huo wa watu 20 pia umewahusisha Naibu Meya Bi. Sarah Kanyike Ssebagala, Waheshimiwa Madiwani na baadhi ya watendaji wa Mamlaka ya Jiji la Kampala.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Anuani ya Posta: S.L.P 20950
Simu ya mezani: 0738 378 386
Namba ya Mkononi: 0738 378 386
Barua Pepe: info@dcc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.