Na: Doina Mwambagi
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Mheshimiwa Edward Mpogolo, amepongeza juhudi za Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam katika kuimarisha utoaji wa mikopo ya asilimia 10 kwa vikundi vya wanawake, vijana, na watu wenye ulemavu,
Mhe. Mpogolo ameeleza kuwa mikopo hiyo ni chombo muhimu cha kufanikisha maono ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuwawezesha wananchi kiuchumi.
Amesema kuwa mapato yaliyokusanywa na Halmashauri yameongezeka , hali iliyoleta mabadiliko makubwa katika uwezo wa Jiji kutoa mikopo kwa walengwa, ambapo zaidi ya shilingi bilioni 18 zinaenda kutolewa kwanzia sasa.
“Fedha hizi si msaada ni haki ya wananchi waliopo kwenye mpango huu wa kisheria. Rais wetu ameweka mazingira wezeshi, sisi kama viongozi ni lazima tusimame imara kuhakikisha fedha hizi zinawafikia walengwa kwa uaminifu na bila urasimu,” amesema DC Mpogolo kwa msisitizo.
Mheshimiwa Mpogolo amewataka wanufaika wa mikopo kuhakikisha wanashiriki kikamilifu katika mafunzo ya ujasiriamali na elimu ya fedha ili kuendesha biashara kwa tija na kuhakikisha urejeshaji wa mikopo unafanyika kwa wakati ili kuwafikia wananchi wengine.
Kwa mwaka wa fedha 2025/2026, Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam inatarajia kutenga zaidi ya shilingi bilioni 22 kwa ajili ya mikopo hiyo, ikiwa ni mwendelezo wa utekelezaji wa maelekezo ya Serikali ya Awamu ya Sita katika kuinua kundi kubwa la wananchi kupitia uchumi jumuishi.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Anuani ya Posta: S.L.P 20950
Simu ya mezani: 0738 378 386
Namba ya Mkononi: 0738 378 386
Barua Pepe: info@dcc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.