Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Mohamed Mchengerwa (Mb) ameeleza kuwa Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan imejipanga kuhakikisha inaendelea kuboresha huduma kwa Watanzania kupitia Mradi wa Uendelezaji Jiji la Dar esSalaam (DMDP) kwa awamu ya pili ukiwa na zaidi ya Shilingi Trilioni 1.18 sawa na Dola za Kimarekani Milioni 447.
Akizungumza wakati wa hafla ya utiaji saini wa mikataba nane ya ujenzi wa miundombinu ya barabara katika Halmashauri tano za Mkoa wa Dar es Salaam kupitia DMDP awamu ya pili leo Octoba 24, 2024 iliyofanyika katika viwanja vya MwembeYanga Temeke Dar es Salaam, Waziri Mchengerwa ameeleza kuwa nia ya Serikali ni kuhakikisha miundombinu inaboreshwa ili wananchi wapate huduma bora na kwa wakati.
Aidha, Mhe. Mchengerwa amesema mradi huo unajumla ya kilometa mraba za lami 250, mifereji yenye kilometa 90, stendi za mabasi tisa pamoja na masoko 18 ambapo kwa hatua ya awali mikataba inayosainiwa inaenda kutekeleza miradi ya barabara zenye urefu wa Km 63.66 zikiwa na thamani ya shilingi bilioni 190 katika Halmashauri tano za Mkoa wa Dar es Salaam huku zabuni 11 zilizobaki zenye jumla ya Km 104.56 zinatarajiwa kukamilika na Mikataba kusainiwa ndani ya Mwezi Novemba.
"Jambo hili linaonesha nia nje ya Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika utekelezaji wa mradi wa uboreshaji wa Jiji la Dar es Salaam, ambapo unatarajiwa kuboresha miundombinu mbalimbali barabara, masoko, vituo vya mabasi pamoja na miradi ya taka ngumu hivyo niwaagize Katibu Mkuu TAMISEMI na Mtendaji Mkuu wa TARURA kuhakikisha mnasimamia vizuri utekelezaji wa miradi hiyo ikamilike kwa wakati na ubora, kwani muda hautaongezwa kwa mkandarasi yoyote asipokamilisha kwa wakati." Amesisitiza Mhe. Mchengerwa.
Sambamba na hilo, Mhe. Mchengerwa amemtaka Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kuhakikisha anawasimamia wakandarasi hao ili waweze kukamisha miradi hiyo kwa wakati huku akiwasisitiza kuhakikisha wanazingatia uhitaji wa wananchi, katika utekelezaji wa mradi hiyo, isijengwe maeneo ambayo sio rafiki na wananchi, hivyo wahakikishe masoko zaidi ya 20 yatakayojengwa yanajengwa penye uhitaji huku akizitaka Halmashauri zote kuhakikisha wanawajengea uwezo wafanya biashara.
Awali akiongea wakati wa hafla hiyo Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Albert Chalamila amemshukuru Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kundelea kuboresha huduma za wananchi kwani miradi hii itaenda kuboresha miundombinu pamoja na kurahisisha usafiri kwa watanzania huku akimuhakikishia kutekeleza yale yote atakayo ya agiza sambamba na kuhakikisha anawasimamia wakandarasi wote ili waweze kukamilisha kazi kwa wakati.
Aidha, kwa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam mradi wa DMDP awamu ya pili kwa mikataba ya awali itaenda kutekeleza mradi wa mkataba mmoja wa barabara za Km 9.2 zenye thamani ya shilingi bilioni 30.3 chini ya Mkandarasi M/s Jiangxi Geo- Engneering Group Corporation Ltd. ambapo barabara hizo ni pamoja na barabara ya Kitunda - Kivule - Msongola yenye urefu wa Km 6.25 na barabara ya Kivule - Majohe Junction yenye urefu wa Km 2.77.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Anuani ya Posta: S.L.P 20950
Simu ya mezani: 0738 378 386
Namba ya Mkononi: 0738 378 386
Barua Pepe: info@dcc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.