Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam Ndugu Elihuruma Mabelya ameahidi kuichangia Shule ya Sekondari Jitegemee kiasi cha Shilingi Milioni 5 na Kompyuta 3 ikiwa ni kuunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya Sita katika kuboresha Mazingira ya ufundishaji katika Shule hiyo.
Mabelya ametoa ahadi hiyo katika mahafali ya 41 ya kidato cha nne yaliofanyika shuleni hapo leo Septemba 26,2025 ambapo jumla ya wahitimu 103 wa Shule hiyo wanatarajiwa kuhitimu kidato cha nne Novemba mwaka huu.
"Natarajia kuwa Wanafunzi hawa watakuwa mabalozi wazuri katika Jamii, kuonesha ufaulu wao kwa kuwa Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan anaendelea kuboresha mazingira ya Elimu nchini, hivyo nawasihi sana mkadumishe nidhamu na kujituma katika masomo yenu". Alisema Mabelya.
Aidha, amewasisitiza wazazi kuhakikisha wanawapa watoto wao malezi bora yakayosababisha kupata elimu bora, viongozi watarajiwa na kuwahakikishia kuwa Serikali inaendelea kuboresha maslahi ya waalimu na miundombinu bora ya utendaji kazi wao ili kupata matokeo mazuri kwa wahitimu.
Kwa upande wake Makamu Mkuu wa Shule hiyo Luteni Kanali Mao Warioba amemuhakikishia Mkurugenzi huyo wa Jiji kuwa wahitimu hao wameandaliwa vyema ili kufanya mtihani wao unaotarajiwa kufanyika novemba mwaka huu pia hawana waswasi kuwa watafaulu kutokana na maandalizi mazuri.
Mkurugenzi wa Jiji la Dar es salaam ni mmoja wa wanafunzi waliopata elimu ya Sekondari katika shule ya Sekondari ya Jitegemee.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Anuani ya Posta: S.L.P 20950
Simu ya mezani: 0738 378 386
Namba ya Mkononi: 0738 378 386
Barua Pepe: info@dcc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.