Leo, Septemba 16,2025, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, Ndugu Elihuruma Mabelya, kwa niaba ya watumishi wa Jiji, ametoa salamu za pole kwa Makamu Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Wasichana Kisutu, Mwalimu Sophia Charles Makange, kufuatia kifo cha mume wake na watoto wake wanne.
Mkurugenzi Mabelya ametoa salamu hizo katika ibada ya kuaga miili ya marehemu, iliyofanyika Kanisa la KKKT Kijitonyama, kabla ya kusafirishwa kwenda Jijini Tanga kwa ajili ya maziko.
Mabelya amesema kuwa Serikali ipo bega kwa bega na familia hiyo katika kipindi hiki kigumu, kuhakikisha wanapata faraja na msaada wa karibu siku hadi siku.
“Mwl. Sophia ni mtumishi mwenzetu ambaye anakabiliana na majonzi makubwa. Sisi, kama familia ya watumishi wa Jiji, tupo pamoja naye kumpa faraja na msaada kwenye kipindi hiki kigumu." alisema Mabelya
Ikumbukwe kuwa vifo hivyo vilitokana na ajali ya gari iliyotokea Septemba 14 2025, eneo la Msata mkoani Pwani.
Mungu azilaze roho za marehemu mahali pema peponi. Amina.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Anuani ya Posta: S.L.P 20950
Simu ya mezani: 0738 378 386
Namba ya Mkononi: 0738 378 386
Barua Pepe: info@dcc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.