Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam Elihuruma Mabelya amewataka Mameneja wa vyanzo vya mapato na wakuu wa kanda kufanya kazi kwa ushirikiano katika ukusanyaji wa mapato ili kufikia lengo la kukusanya Bilioni 130 kwa mwaka wa fedha 2024/2025.
Hayo yamebainishwa Leo tarehe 23 Agosti 2024, na Mkurugenzi wa Jiji wakati wa kikao na mameneja wa vyanzo vya mapato na wakuu wa kanda katika Ukumbi wa Arnatoglou, Ili kujadili changamoto na mbinu mbalimbali katika ukisanyaji wa mapato.
Aidha, Mkurugenzi Mabelya amewasisitiza watumishi hao kufanya kazi kwa bidii, kujituma huku akiwahakikishia kuwapa ushirikiano wa hali na mali.
“Nina taarifa zenu kuwa mnafanya vizuri katika ukisanyaji wa mapato , hivyo niwaombe tuendeleze kasi hiyo hiyo Ili tuweze kufikia bajeti yetu ya Bilioni 130 ili Tuweze kuwaletea maendeleo wananchi wetu katika sekta za Afya, Elimu, na miundombinu ikiwemo Barabara” Amesisitiza Mabelya.
Sambamba na hilo, amesema ni muhimu kutoa Elimu ya kodi kwa wafanyabiashara wa Jiji la DSM Ili waweze kulipa kodi kwa wakati kwa maendeleo chanya kwa wananchi.
Awali mameneja wa vyanzo vya mapato na wakuu wa kanda waliwasilisha changamoto wanazokutana nazo na kuomba kuwe na vikao vya mapato Ili waweze kujadili changamoto na mbinu mbalimbali za kuweza kuongeza ukusanyaji mapato kwa Serikali.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Anuani ya Posta: S.L.P 20950
Simu ya mezani: 0738 378 386
Namba ya Mkononi: 0738 378 386
Barua Pepe: info@dcc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.