• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Dar es Salaam City Council
Dar es Salaam City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Jiji
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Fedha, Utawala na Utumishi
      • Ujenzi na Zimamoto
      • Udhibiti Taka
      • Mipangomiji, Mazingira na Usafirishaji
      • Afya na Huduma za Tiba
    • Vitengo
      • Mipango, Ufuatiliaji na Takwimu
      • Sheria na Usalama
      • Itifaki, Uhusiano na Umma
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Ugavi na Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Shughuli za Utalii
      • Dar es Salaam Yetu
      • Misitu na Mashamba ya wanyama wafugwao
      • Sehemu za kitamaduni, ngoma za asili na sanaa za mikono
      • Kituo cha Urithi wa Ubunifu Majengo na Utalii
      • Maeneo ya kupumzika, bustani na viwanja vya michezo
      • Maeneo ya Manunuzi
      • Majengo na maeneo ya kihistoria
      • Uwanda wa bahari, fukwe na visiwa
    • Urejelezaji wa Taka Ngumu
  • Huduma Zetu
    • Vibali vya Pikipiki
    • Vibali vya Maegesho ya Teksi
    • Vibali vya Kuingiza Magari ya Mizigo
    • Vituo Vikuu vya Mabasi
    • Udhibiti Taka Ngumu
    • Taarifa za Historia ya Viwanja
    • Mazishi ya miili ya marehemu wasiokuwa na ndugu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha na Uongozi
      • Kamati ya Mipangomiji, Mazingira na Miundombinu
      • Kamati ya Mipango na Ufuatiliaji
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba ya Vikao vya Kisheria
    • Ratiba ya Mstahiki Meya
    • Mameya Wazamani wa Jiji
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi iliyo kwenye Mpango
    • Miradi Inayoendelea
    • Vitega Uchumi vya Jiji
  • Machapisho
    • Sheria
    • Sheria Ndogo
    • Sera
    • Miongozo
    • Taarifa mbalimbali
    • Fomu za Maombi
    • Fomu za Ahadi ya Uadilifu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Hotuba
    • Habari Mpya
    • Matukio

RC DSM aridhishwa na utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Jiji la DSM

Tarehe iliyowekwa: June 28th, 2023

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Albert Chalamila aridhishwa na matumizi ya fedha na kasi ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kupitia fedha toka Serikali Kuu pamoja na fedha za mapato ya ndani ya Halmashauri.

Hayo ameeleza leo tarehe 28 Juni, 2023 Jijini Dar es Salaam wakati wa ziara ya kukagua utekelezaji wa miradi mbalimlbali ya maendeleo inayotekelezwa na Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kwa mwaka 2022/2023 lengo likiwa ni kuhakikisha Ilani ya Chama cha Mapinduzi inatekelezwa kwa kasi zaidi.

Miradi iliyotembelewa na Mkuu wa Mkoa ni pamoja na ukamilishaji wa ujenzi wa madarasa ya ghorofa 5 katika shule ya Sekondari Liwiti itakayogharimu takribani shilingi bilioni 1.57 pindi likikamilika, ukaguzi wa ujenzi wa Shule Mpya ya Msingi Kivule Mpya yenye madarasa 14 na matundu 16 ya vyoo ambapo ujenzi huo upo hatua ya umaliziaji na hadi kufikia Juni 30, 2023 ujenzi unatarajiwa kukamilika na utagharimu takribani shilingi milioni 475.3 zikiwa ni fedha kutoka mradi wa Boost pamoja na ukaguzi wa mradi wa ujenzi wa Kituo cha Afya Zingiziwa wenye thamani ya shilingi milioni 500 zikiwa ni fedha za mapato ya ndani ya Halmashauri.

Akizungumza na wananchi baada ya kukagua mradi Mhe. Chalamila alisema ili kuacha alama Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan aliamua kuwekeza nguvu zaidi katika sekta ya elimu na Afya ili wananchi wapate huduma bora kwa ukaribu zaidi na kwa wakati.

“Napenda kuwapongeza viongozi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kwa ufuatiliaji na usimamizi mzuri wa miradi kwani kupitia miradi hii changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi zitakuwa zimetatuliwa kwa kiasi kwani mmejengewa vituo vya afya pamoja na shule maeneo ya Karibu zaidi hivyo naamini ukaribu wa huduma hizi utapunguza adha mbalimbali zikiwemo toro kwa wanafunzi pamoja na vifo vya uzazi, niwaombe mtumie vizuri rasilimali hizi na kwa changamoto ndogondogo tutaendelea kuzitatua na mambo yatakua mazuri zaidi." Ameeleza Mhe. Chalamila.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Edward Mpogolo ametoa shukurani zake kwa Mkuu wa Mkoa kwa Ziara aliyoifanya ya kukagua miradi ya Maendeleo pamoja na kuongea na wananchi huku akimuhakikishia kutekeleza yote aliyoyaagiza.

Matangazo

  • TAARIFA KWA UMMA February 19, 2025
  • TAARIFA KWA UMMA - MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA January 17, 2025
  • MATOKEO YA UPIMAJI WA KITAIFA WA DARASA LA NNE (SFNA) 2024 January 04, 2025
  • UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA, 2025 December 16, 2024
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • "Tutahakikisha tunasimamia Kata 36 na Mitaa 159 ili Jiji la DSM liwe safi" - DC Mpogolo

    May 03, 2025
  • Jiji La DSM laweka mikakati kushinda UMITASHUMTA ngazi ya Mkoa

    April 29, 2025
  • Wakazi wa Jiji la Dar es Salaam waadhimisha Muungano kwa kupanda miti na kufanya usafi wa mazingira

    April 26, 2025
  • Zoezi la usafi wa mwisho wa wiki laendelea

    April 12, 2025
  • Angalia zote

Video

Msimbazi Basin Development Project Implementation Area
Video Zingine

Viunganishi vya Haraka

  • Mameya wa zamani wa Jiji
  • Vibali vya kuingia na Pikipiki katikati ya Jiji
  • Udhibiti wa Taka ngumu Jijini
  • Eneo Maalum la Usafi Jijini
  • Kituo cha Urithi wa Ubunifu Majengo na Utalii
  • Uwanda wa Bahari, Fukwe na Visiwa
  • Sehemu za Kitamaduni, Ngoma za Asili na Sanaa za Mikono
  • Majengo na Maeneo ya Kihistoria
  • Maeneo ya Kupumzika, Bustani na Viwanja vya Michezo

Viunganishi Linganifu

  • BUNGE
  • Blogu ya Jiji
  • UTUMISHI
  • IKULU
  • TAMISEMI
  • IDARA YA HABARI MAELEZO

Wasomaji mbalimbali duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM

    Anuani ya Posta: S.L.P 20950

    Simu ya mezani: 0738 378 386

    Namba ya Mkononi: 0738 378 386

    Barua Pepe: info@dcc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.