Na: Amanzi Kimonjo & Judith Msuya
Mkuu wa Wilaya wa Ilala Mhe.Ng'wilabuzu Ndatwa Ludigija leo tarehe 21 february 2022 amefanya ziara ya kutembelea Kata ya Zingiziwa ambako Wilaya ya Ilala imepakana na Wilaya ya Kisarawe lengo likiwa ni kuweka sawa suala la Mipaka hiyo kwa wananchi wa eneo la Ngobedi 'B'.
Aidha katika ziara hiyo iliyohudhuriwa na Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam pamoja na wataalamu wa Mipango miji na ardhi wa Wilaya zote mbili waliweza kujiridhisha na kuazimia kua kutokana na mipaka ya nchi eneo hilo la Ngobedi 'B' lipo Wilaya ya Kisarawe.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe.Ngw'ilabuzu Ludigija amesema "mgogoro huu umekua wa muda mrefu na sisi tumeukuta lakini kwa dhamira njema tumeona tuweke mambo sawa hivyo tumekaa na wataalamu wetu na wamejiridhisha kwamba eneo hili la Ngobedi 'B' liko Wilaya ya Kisarawe, kwahiyo niwaombe sana wananchi, sisi wakuu wa wilaya hatubadilishi mipaka ya nchi, kazi yetu ni Utawala ili tuweze kuwahudumia wananchi vizuri hivyo mpaka kufikia wiki ijayo wataalamu wetu watakua washaainisha hiyo mipaka na hii itatusaidia zaidi kwenye suala zima la ulinzi na uslama hivyo niwaombeni sana, sisi wakuu wenu wa Wilaya tutaendelea kushirikiana ili muweze kufikiwa na huduma za Kijamii."
Aidha ziara hiyo haikuishia hapo iliendelea katika Soko la Zingiziwa ambapo Mhe. Ludigija aliweza kuongea na wananchi wa soko hilo lengo likiwa ni kuwaelekeza na kuwakumbusha wote waliorudi kufanya biashara maeneo yasiyo rasmi warudi sokoni kwani wakirudi sokoni itakua rahisi kufikiwa na huduma za kijamii.
Sambamba na hilo Mhe. Ludigija ametoa maelekezo kwa wafanyabiashara wote wanarudi kufanya biashara Maeneo yasiyo rasmi warudi sokoni kabla hawajachukuliwa hatua. "Kwanza napenda kumshukuru Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam kwa fedha alizotoa kwa ujenzi wa soko la zingiziwa hivyo niwaombe wananchi wote wa soko la Zingiziwa wanarudi kufanya biashara maeneo ya barabarani warudi sokoni hivyo niwaombe sana tufanye biashara hapa sokoni bila kurudi barabarani tusingependa sisi Serikali kuumiza wananchi wetu kwakutumia nguvu hivyo tunawaomba mfanye biashara sokoni kwani fedha zinazotolewa kwaajili ya kujenga masoko zinatolewa kusudi wafanyabiashara wetu mfanye biashara sehemu rasmi na salama pia kama mnataka kujenda frame wenyewe muwasiliane na Kamati ya maendeleo ya Kata ya Zingiziwa ili mpatiwe ramani mjenge na mfanye biashara zenu kwa uhakika zaidi." amesema Mhe. Ludigija.
Akiongea kwa niaba ya wananchi wa Kata ya Zingiziwa Diwani wa Kata ya Zingiziwa Mhe. Maige Amesema "kwanza napenda kutoa shukurani zangu za dhati kwa Mkurugunzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kwa kutupatia kiasi cha shilingi milioni 100 kwa ajili ya ujenzi wa soko letu la Zingiziwa hivyo niwaombe wananchi wa Kata ya Zingiziwa kuwa wavumilivu kwani huduma za jamii zote zitatufikia na pia niwasihi tuendelee kubaki sokoni kwani ndiyo sehemu salama kwaajili ya kufanya biashara zetu kwa kujipatia kipato na kuiongezea Halmashauri yetu pato la ndani."
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Anuani ya Posta: S.L.P 20950
Simu ya mezani: 0738 378 386
Namba ya Mkononi: 0738 378 386
Barua Pepe: info@dcc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.