Na Judith Damas, Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Mhe Omary Kumbilamoto ameahidi kuboresha miundombinu katika kata zote za Halmashauri ya Jiji , amesema hayo katika ziara yake ya kutembelea shule ya msingi Magoza iliyopo Kata ya Kisukuru leo tarehe 3, Machi 2021 ambapo amekabidhi vifaa vya ujenzi vyenye thamani ya shilingi laki nane na themanini (880000) ikiwemo masinki 30 ya vyoo pamoja na mifuko20 ya saruji hivyo vifaa hivyo viligawanywa kama ifuatavyo,mifuko 10 ya saruji na masinki 14 ya vyoo katika shule ya msingi Magoza pamoja na mifuko 10 ya saruji na masinki 16 ya vyoo katika shule ya msingi Vingunguti.
Akizungumza na wananchi wa Kata ya Kisukuru pamoja na walimu wa shule ya msingi Magoza Mstahiki Meya amemshukuru Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt John Pombe Magufuli kwa kuipandisha hadhi iliyokua Manispaa ya Ilala kuwa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam na kumuahidi Rais kuwa hatomuangusha.
"Namshukuru Mhe.Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli kwa heshima aliyotupa na kutukabidhi Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kutoka Manispaa ya Ilala na sisi kama wasaidizi wake ni kuhakikisha tunatekeleza malengo yote ya Rais aliyokuwa nayo hivyo changamoto nyingine ndogodogo tunaahidi tutazitatua".Amesema, Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam.
Aidha, Kaimu Afisa Elimu Msingi Bw.Abilah Magochi Mchia amemshukuru Msathiki Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kwa kutoa msaada wa masinki 14 ya vyoo na mifuko ya simenti 10 katika shule ya msingi Magoza pamoja na masinki 16 katika shule ya msingi Vingunguti kwani ni msaada mkubwa ambao utaboresha maendeleo katika shule hizo .
“Tunakushukuru sana Msahiki Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam Mhe. Omary Kumbilamoto kwa kuleta msaada katika shule zetu za msingi za Magoza pamoja na Vingunguti ni msaada mkubwa sana ambao utaboresha shule zetu hizi kwani vyoo vya wanafunzi vilikua haviko katika kiwango kizuri lakini kwa masinki haya watoto wetu wataenda kutumia vyoo vya kisasa ambavyo vipo katika mazingira salama kwamaana hawatoweza kupata magonjwa ya maambukizi”.Amema kaimu Afisa Elimu Msingi Bw.Mchia
Sambanba na hilo, Kaimu Afisa Elimu Msingi Bw.Mchia amemshukuru Mheshimiwa diwani Lucy Jeremiah Lugome wa Kata ya Kisukuru kwa kueleza Changamoto hiyo kwa Mstahiki Meya ili zifanyiwe kazi.
“Umemueleza Mstahiki Meya Changamoto iliyokua inaikabili shule ya Msingi Magoza basi Mstahiki Meya kwa umuhimu amesisitiza kujengwa vyumba vinne vya madarasa katika shule hii ya Msingi Magoza na Mstahiki Meya nakuahidi hizo fedha zitaletwa hapa kwaajili ya kuanza ujenzi wa vyumba hivyo vinne vya madarasa”.Amesema hayo Kaimu Afisa Elimu Msingi
Kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Magoza Bw. Simeon Kahwa amesema msaada huu uliotolewa na Mstahiki Meya utasaidia sana kuleta mazingira rafiki kwa wanafunzi kwani wataongeza idadi ya vyoo ambavyo vitasaidia kulinda afya za wanafuzi.
“Tunamshukuru sana Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam kutuletea msaada huu kwani kimsingi idadi ya vyoo ilikua haitoshelezi kwa wanafunzi hivyo kutokana na msaada huu tutaongeza idadi ya vyoo kwa ajili ya kuleta mazingira rafiki kwa watoto wetu”.Amesema Mwl.Kahwa
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Anuani ya Posta: S.L.P 20950
Simu ya mezani: 0738 378 386
Namba ya Mkononi: 0738 378 386
Barua Pepe: info@dcc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.