Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa - TAMISEMI (Afya) Dkt. Wilson Mahera Charles amekagua ujenzi wa Kituo cha Afya Mchikichini na kuridhishwa na maendeleo ya ujenzi huo.
Akiongea wakati wa ukaguzi, Dkt. Charles amemtaka Mhandisi kusimamia kwa ukamilifu ujenzi wa mradi huo ili urahisishe upatikanaji wa huduma za afya kwani wananchi wanasubiri kunufaika na adhma ya Mhe. Rais ya kuimarisha miundombinu pamoja na kutoa huduma bora kwa Jamii.
"Niwapongeze Jiji la Dar es Salaam kwa ujenzi wa kituo hichi kwani kitapunguza msongamano kwenye hospitali za karibu za Mnazi Mmoja na Amana na kitasogeza huduma muhimu ya afya karibu zaidi kwa wananchi." Amesema Dkt. Charles.
Naye, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Dkt. Rashid Mfaume ameahidi kuyafanyia kazi maelekezo yaliyotolewa na na kusimamia ujenzi wa Kituo hicho kwa karibu.
Kituo cha Afya cha Mchikichini kinajengwa kwa gharama ya Tsh. Bilioni 5.2 fedha kutoka mapato ya ndani ya Halmashauri na kinatarajiwa kukamilika mwezi Novemba, 2023.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Anuani ya Posta: S.L.P 20950
Simu ya mezani: 0738 378 386
Namba ya Mkononi: 0738 378 386
Barua Pepe: info@dcc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.