• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Dar es Salaam City Council
Dar es Salaam City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Jiji
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Fedha, Utawala na Utumishi
      • Ujenzi na Zimamoto
      • Udhibiti Taka
      • Mipangomiji, Mazingira na Usafirishaji
      • Afya na Huduma za Tiba
    • Vitengo
      • Mipango, Ufuatiliaji na Takwimu
      • Sheria na Usalama
      • Itifaki, Uhusiano na Umma
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Ugavi na Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Shughuli za Utalii
      • Dar es Salaam Yetu
      • Misitu na Mashamba ya wanyama wafugwao
      • Sehemu za kitamaduni, ngoma za asili na sanaa za mikono
      • Kituo cha Urithi wa Ubunifu Majengo na Utalii
      • Maeneo ya kupumzika, bustani na viwanja vya michezo
      • Maeneo ya Manunuzi
      • Majengo na maeneo ya kihistoria
      • Uwanda wa bahari, fukwe na visiwa
    • Urejelezaji wa Taka Ngumu
  • Huduma Zetu
    • Vibali vya Pikipiki
    • Vibali vya Maegesho ya Teksi
    • Vibali vya Kuingiza Magari ya Mizigo
    • Vituo Vikuu vya Mabasi
    • Udhibiti Taka Ngumu
    • Taarifa za Historia ya Viwanja
    • Mazishi ya miili ya marehemu wasiokuwa na ndugu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha na Uongozi
      • Kamati ya Mipangomiji, Mazingira na Miundombinu
      • Kamati ya Mipango na Ufuatiliaji
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba ya Vikao vya Kisheria
    • Ratiba ya Mstahiki Meya
    • Mameya Wazamani wa Jiji
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi iliyo kwenye Mpango
    • Miradi Inayoendelea
    • Vitega Uchumi vya Jiji
  • Machapisho
    • Sheria
    • Sheria Ndogo
    • Sera
    • Miongozo
    • Taarifa mbalimbali
    • Fomu za Maombi
    • Fomu za Ahadi ya Uadilifu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Hotuba
    • Habari Mpya
    • Matukio

"Tutazingatia sheria na kanuni katika utoaji wa mikopo" - Mkurugenzi Mabelya

Tarehe iliyowekwa: February 24th, 2025

Na: Doina Mwambagi

Mkurugenzi  wa Halmashauri Jiji la Dar es Salaam, Ndugu Elihuruma Mabelya  amesema kuwa Jiji la Dar es Salaam litaendelea kuzingatia sheria na kanuni zote za utoaji wa mikopo ili kuhakikisha kuwa fedha zinazotolewa zinawanufaisha walengwa .

Hayo ameyasema Leo februari 24, 2025 wakati wa mkutano maalumu wa utambulisho wa benki katika usimamizi wa utoaji wa mikopo halmashauri ya jiji uliofanyika katika ukumbi wa Anartoglou Jijini humo.

Mkurugenzi Mabelya  ameeleza kuwa mikopo hiyo inalenga kuwawezesha wanawake, vijana na watu wenye ulemavu kujikwamua kiuchumi kwa kuwapa fursa ya kujiajiri pamoja na kukuza biashara zao.

“Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, kwa kushirikiana na benki za CRDB na NMB, tumejipanga kuhakikisha kwamba mikopo inatolewa kwa kufuata kanuni na taratibu ili iwafikie walengwa sahihi. Hatutabaki kwenye maneno pekee, bali tumejizatiti kutekeleza hili kwa vitendo. Hadi kufikia Februari 12, tumepokea jumla ya maombi 945, na kwa sasa tuko katika hatua ya kuyachambua kwa kina ili kuhakikisha kila anayestahili anapata fursa hii .” Amesisitiza Mabelya

Sambamba na hilo, Ndugu Mabelya amesema kuwa Halmashauri itahakikisha inafanya ufuatiliaji wa karibu kwa wanufaika wa mikopo ili kuhakikisha fedha hizo zinatumika kwa malengo yaliyokusudiwa. Huku  akiwataka wanufaika kurejesha mikopo kwa wakati, hivyo kutoa fursa kwa wengine kunufaika na mfuko huo na kuendeleza mzunguko wa uwezeshaji kiuchumi.

Kwa upande wa benki zilizotambuliwa, wawakilishi wake wamesema kuwa wamepewa jukumu hilo na watalitekeleza kwa weledi na kasi, kwa kushirikiana na maafisa mikopo wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam.

Serikali iliisimamisha mikopo hiyo ya 10% ili kufanya maboresho, na sasa imechagua Halmashauri 10 za mfano, ikiwemo Jiji la Dar es Salaam na tayari imeingia makubaliano na benki mbili ya CRDB na benki ya NMB kwa ajili ya utoaji wa mikopo hiyo, huku shilingi bilioni 15 zikiwa zimetengwa kwa ajili ya Mikopo kutoka kwenye mapato ya ndani na marejesho ya mikopo ya awali. Hatua hii inalenga kuhakikisha kuwa wanufaika wanapata fursa bora zaidi za mikopo kwa maendeleo yao.

Matangazo

  • TAARIFA KWA UMMA February 19, 2025
  • TAARIFA KWA UMMA - MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA January 17, 2025
  • MATOKEO YA UPIMAJI WA KITAIFA WA DARASA LA NNE (SFNA) 2024 January 04, 2025
  • UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA, 2025 December 16, 2024
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • "Tutahakikisha tunasimamia Kata 36 na Mitaa 159 ili Jiji la DSM liwe safi" - DC Mpogolo

    May 03, 2025
  • Jiji La DSM laweka mikakati kushinda UMITASHUMTA ngazi ya Mkoa

    April 29, 2025
  • Wakazi wa Jiji la Dar es Salaam waadhimisha Muungano kwa kupanda miti na kufanya usafi wa mazingira

    April 26, 2025
  • Zoezi la usafi wa mwisho wa wiki laendelea

    April 12, 2025
  • Angalia zote

Video

Msimbazi Basin Development Project Implementation Area
Video Zingine

Viunganishi vya Haraka

  • Mameya wa zamani wa Jiji
  • Vibali vya kuingia na Pikipiki katikati ya Jiji
  • Udhibiti wa Taka ngumu Jijini
  • Eneo Maalum la Usafi Jijini
  • Kituo cha Urithi wa Ubunifu Majengo na Utalii
  • Uwanda wa Bahari, Fukwe na Visiwa
  • Sehemu za Kitamaduni, Ngoma za Asili na Sanaa za Mikono
  • Majengo na Maeneo ya Kihistoria
  • Maeneo ya Kupumzika, Bustani na Viwanja vya Michezo

Viunganishi Linganifu

  • BUNGE
  • Blogu ya Jiji
  • UTUMISHI
  • IKULU
  • TAMISEMI
  • IDARA YA HABARI MAELEZO

Wasomaji mbalimbali duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM

    Anuani ya Posta: S.L.P 20950

    Simu ya mezani: 0738 378 386

    Namba ya Mkononi: 0738 378 386

    Barua Pepe: info@dcc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.