• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Dar es Salaam City Council
Dar es Salaam City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Jiji
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Fedha, Utawala na Utumishi
      • Ujenzi na Zimamoto
      • Udhibiti Taka
      • Mipangomiji, Mazingira na Usafirishaji
      • Afya na Huduma za Tiba
    • Vitengo
      • Mipango, Ufuatiliaji na Takwimu
      • Sheria na Usalama
      • Itifaki, Uhusiano na Umma
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Ugavi na Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Shughuli za Utalii
      • Dar es Salaam Yetu
      • Misitu na Mashamba ya wanyama wafugwao
      • Sehemu za kitamaduni, ngoma za asili na sanaa za mikono
      • Kituo cha Urithi wa Ubunifu Majengo na Utalii
      • Maeneo ya kupumzika, bustani na viwanja vya michezo
      • Maeneo ya Manunuzi
      • Majengo na maeneo ya kihistoria
      • Uwanda wa bahari, fukwe na visiwa
    • Urejelezaji wa Taka Ngumu
  • Huduma Zetu
    • Vibali vya Pikipiki
    • Vibali vya Maegesho ya Teksi
    • Vibali vya Kuingiza Magari ya Mizigo
    • Vituo Vikuu vya Mabasi
    • Udhibiti Taka Ngumu
    • Taarifa za Historia ya Viwanja
    • Mazishi ya miili ya marehemu wasiokuwa na ndugu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha na Uongozi
      • Kamati ya Mipangomiji, Mazingira na Miundombinu
      • Kamati ya Mipango na Ufuatiliaji
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba ya Vikao vya Kisheria
    • Ratiba ya Mstahiki Meya
    • Mameya Wazamani wa Jiji
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi iliyo kwenye Mpango
    • Miradi Inayoendelea
    • Vitega Uchumi vya Jiji
  • Machapisho
    • Sheria
    • Sheria Ndogo
    • Sera
    • Miongozo
    • Taarifa mbalimbali
    • Fomu za Maombi
    • Fomu za Ahadi ya Uadilifu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Hotuba
    • Habari Mpya
    • Matukio

Uzinduzi wa Kituo cha Urithi wa Ubunifu Majengo na Utalii katika Jiji la Dar es Salaam

Tarehe iliyowekwa: June 30th, 2017

NAIBU Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bibi. Nuru Milao  ameupongeza Uongozi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kwa kulitoa jengo la kale la Old Boma ambalo lina zaidi ya miaka 160 liweze kutumika kama Kituo cha Urithi wa Ubunifu wa Majengo na Utalii. 

Jengo la Old Boma lenye historia kubwa katika nchi yetu ambalo limefanyiwa ukarabati kwa kiwango cha juu na kuwa mfano wa uhifadhi endelevu na kituo cha kutangaza historia ya ukuaji wa miji yetu kanda ya Afrika Mashariki kwa ufadhili wa Umoja wa Nchi za Ulaya.

Akizungumza katika hafla ya kufungua kituo hicho leo Jijini Dar es Salaam kwa niaba ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt.Harrison Mwakyembe (MB), Milao alisema hatua hiyo inadhihirisha dhamira ya Serikali ya kuhakikisha kuwa utamaduni wa Mtanzania unadumishwa na kukuzwa.

Hafla hiyo imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali, Waheshimiwa Madiwani wa Jiji la Dar es Salaam wakiongozwa na Mstahiki Meya wa Jiji Isaya Mwita Charles, Balozi wa Umoja wa Nchi za Ulaya, Balozi wa Ufaransa, wananchi na wadau mbalimbali wa Jiji la Dar es Salaam.

Mgeni rasmi pia amesifu juhudi zinazofanywa na Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam za kuvitangaza vivutio vya utalii jijini kwa lengo la kuogeza pato kupitia shughuli za utalii na mipango yake ya kuwa na mabasi ya Halmashauri ya kuhudumia watalii.

Bi. Nuru pia ametoa pongezi kubwa kwa Jumuiya ya Wabunifu Majengo Tanzania na washirika wake kwa juhudi wanazofanya za kuanzisha mpango wa kuelimisha, kutunza na kudumisha majengo ya kale ambayo utakua ukisaidia kukuza na kuendeleza utalii katika Jiji la Dar es Salaam na Tanzania kwa ujumla.

Akihitimisha hotuba yake mgeni rasmi ametoa wito kwa wananchi na wadau wote kuwa na mawazo ya utunzaji wa majengo ya kale badala ya uvunjwaji wa majengo hayo kama inavyoendelea katika Jiji la Dar es Salaam bila kupata vibali vya mamlaka husika Serikalini.

Mgeni rasmi ametoa msisitizo kwa Mamlaka za Serikali za Mitaa katika Jiji la Dar es Salaam  wa kusimamia sheria na kushughulikia kero zinazotokana na udhaifu wa kutosimamia sheria ambazo kimsingi zingeweza kusaidia kuimarisha usalama na kutunza mazingira ya majengo yote ya kale na majengo ya kisasa ambayo ni sehemu kubwa ya vivutio vya utalii nchini.

Naye  Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam Mhe. Isaya Mwita Charles ameeleza kuwa kufunguliwa kwa kituo hiko ni fursa ya kukuza pato la uchumi la wakazi wa Jiji la Dar es Salaam na taifa kwa ujumla kupitia mapato ya watalii watakaokitembelea.

"Tayari tumeweka mipango mbalimbali ya kukuza, kuhifadhi, kutangaza vivutio vya utalii tulivyonavyo na kuvifanya kuwa vyanzo vikubwa vya mapato katika Jiji letu ikiwemo utoaji mafunzo kwa madereva Teksi ambao wanahusika katika kuwasafirisha  watalii ili wawe na uelewa zaidi kuhusu kituo hiki” alisema Mstahiki Meya wa Jiji.

Kwa Upande wake Balozi wa Umoja wa Nchi za Ulaya Mhe. Roeland Van De Geer amesema ofisi yake iko tayari kushirikiana kwa karibu na Jiji la Dar es Salaam na Tanzania katika kukuza na kuendeleza majengo ya kale na katika kuleta maendeleo kwa ujumla.

Matangazo

  • TAARIFA KWA UMMA February 19, 2025
  • TAARIFA KWA UMMA - MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA January 17, 2025
  • MATOKEO YA UPIMAJI WA KITAIFA WA DARASA LA NNE (SFNA) 2024 January 04, 2025
  • UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA, 2025 December 16, 2024
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • "Tutahakikisha tunasimamia Kata 36 na Mitaa 159 ili Jiji la DSM liwe safi" - DC Mpogolo

    May 03, 2025
  • Jiji La DSM laweka mikakati kushinda UMITASHUMTA ngazi ya Mkoa

    April 29, 2025
  • Wakazi wa Jiji la Dar es Salaam waadhimisha Muungano kwa kupanda miti na kufanya usafi wa mazingira

    April 26, 2025
  • Zoezi la usafi wa mwisho wa wiki laendelea

    April 12, 2025
  • Angalia zote

Video

Msimbazi Basin Development Project Implementation Area
Video Zingine

Viunganishi vya Haraka

  • Mameya wa zamani wa Jiji
  • Vibali vya kuingia na Pikipiki katikati ya Jiji
  • Udhibiti wa Taka ngumu Jijini
  • Eneo Maalum la Usafi Jijini
  • Kituo cha Urithi wa Ubunifu Majengo na Utalii
  • Uwanda wa Bahari, Fukwe na Visiwa
  • Sehemu za Kitamaduni, Ngoma za Asili na Sanaa za Mikono
  • Majengo na Maeneo ya Kihistoria
  • Maeneo ya Kupumzika, Bustani na Viwanja vya Michezo

Viunganishi Linganifu

  • BUNGE
  • Blogu ya Jiji
  • UTUMISHI
  • IKULU
  • TAMISEMI
  • IDARA YA HABARI MAELEZO

Wasomaji mbalimbali duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM

    Anuani ya Posta: S.L.P 20950

    Simu ya mezani: 0738 378 386

    Namba ya Mkononi: 0738 378 386

    Barua Pepe: info@dcc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.