Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, kupitia Idara ya Maendeleo ya Jamii, imefanya mafunzo maalumu kwa vikundi vilivyoomba mikopo ya asilimia 10 ambavyo vinakumbwa na changamoto mbalimbali.
Mafunzo hayo yametolewa leo Septemba 18, 2025 katika Ukumbi wa Drimpu Jijini Dar es Salaam, ili kuhakikisha vikundi hivyo vinafanya marekebisho ya makosa yaliyojitokeza wakati wa mchakato wa uombaji wa Mikopo hiyo.
Akizungumza katika mafunzo hayo, Afisa Maendeleo ya Jamii wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, Bi. Rahma Athumani, amesema lengo la Serikali ni kuhakikisha makundi ya watu wenye ulemavu, Vijana, na Wanawake wanapata mikopo hiyo.
“Kuna baadhi ya changamoto zinazokabili vikundi katika mchakato huu kama vile maandiko ya miradi yasiyo sahihi, kutumia biashara ya mtu mmoja kama msingi wa kikundi, kukosa leseni, kutokuwa na vitambulisho vya wajasiriamali, pamoja na tofauti kati ya mradi waliouombea mkopo na mradi wanaotekeleza, hivyo tumeona ni bora tuwakusanye wote tuwape elimu kwa pamoja”. Alisem Bi. Rahma.
Aidha amesema vikundi hivyo vimepewa muda wa siku 14 kuhakikisha wanarekebisha changamoto zao, huku akibainisha kuwa timu ya Mikopo itakuwa ikiwafuatilia na kutoa msaada ili kuhakikisha wanarekebisha makosa yao na hatimaye kupata mikopo.
Sambamba na hilo ameishukuru benki ya CRDB kwa kwa ushirikiano wao wa karibu katika kuhakikisha vikundi hivyo vinafanikiwa kufikia malengo yao.
Mikopo ya asilimia 10 ni takwa la kisheria ambapo Halamashauri inapaswa kutoa kiasi cha asilimia 10 kutoka kwenye mapato yake ya ndani na kutoa mikopo isiyo na riba kwa makundi ya Vijana, Wanawake na Makundi ya watu wenye ulemavu.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Postal Address: S.L.P 20950
Telephone: 0738 378 386
Mobile: 0738 378 386
Email: info@dcc.go.tz
Copyright © 2017 Dar es Salaam City Council . All rights reserved.