Wananchi wameaswa kuzingatia lishe bora ili kuepukana na magonjwa yasioambukiza, hayo yamesemwa leo Julai 22, 2024 na Mkurugenzi wa Taasisi ya Elimu na Lishe Tanzania Dkt. Ester Nkuba katika halfa ya kuhitimisha kampeni ya lishe Bora kwa njia ya daladala iliyofanyika katika Soko la Kisutu.
Akiongea katika halfa hiyo, Dkt. Nkuba amesema “Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassani amekua mstari wa mbele kupambana na ugonjwa wa utapia mlo kwa wananchi, hivyo nasi tunaunga juhudi zake Ili kuhakikisha wananchi wanakua na Afya njema. Kupitia Elimu hii mliyoipata nawaasa kuzingatia lishe Bora Ili kuepukana na magonjwa yasiyoambukizwa.”
Sambamba na hilo, Dkt. Nkuba amesema “Lishe bora ni kula chakula cha kutosha na chakula chenye virutubisho vyote muhimu. Lishe bora husaidia mwili kukua vyema, kuujenga mwili lakini pia huimarisha kinga ya mwili ili kuweza kupigana na magonjwa. Ili iwe bora ni muhimu iwe na mchanganyiko wa Makundi sita ya chakula ambayo ni protini, wanga, fati, mbogamboga, madini, matunda.“
Aidha, Mkurugenzi wa Shirika la Nutrition Connect Tanzania Bi. Jackline Kawiche amewaasa wanufaika wa Elimu ya lishe kuwa mabalozi kwa jamii inayowazunguka ili Elimu iwafikie wananchi wote lengo la elimu hii ni kuhakikisha wananchi wanakua na afya bora.
Awali akimkaribisha mgeni rasmi, Mwenyekiti wa Soko la Kisutu Abdutwaalib Rashid amesema kuwa msingi wa lishe Bora unaanzia sokoni na Soko la Kisutu ni soko mojawapo lenye bidhaa bora za lishe na bei zake ni rafiki.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Anuani ya Posta: S.L.P 20950
Simu ya mezani: 0738 378 386
Namba ya Mkononi: 0738 378 386
Barua Pepe: info@dcc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.