• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Dar es Salaam City Council
Dar es Salaam City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Jiji
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Fedha, Utawala na Utumishi
      • Ujenzi na Zimamoto
      • Udhibiti Taka
      • Mipangomiji, Mazingira na Usafirishaji
      • Afya na Huduma za Tiba
    • Vitengo
      • Mipango, Ufuatiliaji na Takwimu
      • Sheria na Usalama
      • Itifaki, Uhusiano na Umma
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Ugavi na Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Shughuli za Utalii
      • Dar es Salaam Yetu
      • Misitu na Mashamba ya wanyama wafugwao
      • Sehemu za kitamaduni, ngoma za asili na sanaa za mikono
      • Kituo cha Urithi wa Ubunifu Majengo na Utalii
      • Maeneo ya kupumzika, bustani na viwanja vya michezo
      • Maeneo ya Manunuzi
      • Majengo na maeneo ya kihistoria
      • Uwanda wa bahari, fukwe na visiwa
    • Urejelezaji wa Taka Ngumu
  • Huduma Zetu
    • Vibali vya Pikipiki
    • Vibali vya Maegesho ya Teksi
    • Vibali vya Kuingiza Magari ya Mizigo
    • Vituo Vikuu vya Mabasi
    • Udhibiti Taka Ngumu
    • Taarifa za Historia ya Viwanja
    • Mazishi ya miili ya marehemu wasiokuwa na ndugu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha na Uongozi
      • Kamati ya Mipangomiji, Mazingira na Miundombinu
      • Kamati ya Mipango na Ufuatiliaji
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba ya Vikao vya Kisheria
    • Ratiba ya Mstahiki Meya
    • Mameya Wazamani wa Jiji
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi iliyo kwenye Mpango
    • Miradi Inayoendelea
    • Vitega Uchumi vya Jiji
  • Machapisho
    • Sheria
    • Sheria Ndogo
    • Sera
    • Miongozo
    • Taarifa mbalimbali
    • Fomu za Maombi
    • Fomu za Ahadi ya Uadilifu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Hotuba
    • Habari Mpya
    • Matukio

Wanawake wa Mkoa wa DSM wahamasishwa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia

Tarehe iliyowekwa: May 22nd, 2024

Wanawake wa Mkoa wa Dar es Salaam wametakiwa kuwa mabalozi katika matumizi ya Nishati Safi na salama ya kupikia,lengo likiwa ni kuunga mkono jitihada za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan za utunzaji wa Mazingira.

Wito huo umetolewa na Mshauri wa Rais katika masuala ya wanawake na makundi maalumu Dkt. Sophia Mjema, wakati wa Mkutano wa Uzinduzi wa Programu ya ‘Imarisha Uchumi na Mama Samia’ (IMASA) iliyofanyika Leo Mei 22, 2024  katika Ukumbi wa Arnatoglou Jijini Dar es Salaam na kuwakutanisha viongozi mbalimbali wa majukwaa ya uwezeshaji wanawake kiuchumi Mkoa wa Dar es Salaam, Taasisi  na Mashirika binafsi.

Aidha, Dkt. Mjema amesema "Lengo la Serikali ni kuhakikisha kila Mkoa, Wilaya, Kata na Mitaa kunakuwa na sehemu ambapo wananchi wataweza kupata nishati Safi na salama ya kupikia kwani kupitia nishati safi tutahakikisha usalama, uendelevu na urahisi wa upatikanaji wa nishati ya kupikia, kuokoa muda, pamoja na kupunguza gharama za matumizi, athari za kimazingira na kiafya kwa watumiaji. Pia, ni nyenzo muhimu katika kutekeleza makubaliano ya kitaifa na kimataifa yanayolenga kupambana na mabadiliko ya tabianchi na kupunguza uzalishaji wa gesi joto”.

Sambamba na hilo, Dkt. Mjema amemshukuru Rais Jamhuri ri ya Muungano wa Tanzania kwa kuja na mkakati wa matumizi safi ya nishati ya kupikia huku akiwashukuru Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) kwa kuja na Programu ya ‘Imarisha Uchumi na Mama Samia’ ambayo itakua chachu ya kuwakutanisha wanawake na wananchi katika kujadili masuala mbalimbali ya Kiuchumi bila kusahau suala la nishati safi ya kupikia.

Awali akiongea wakati wa Mkutano huo Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam Toba Nguvila amesema “Tunamshukuru Mheshimiwa Rais Jamhuri ri ya Muungano wa Tanzania kwa kuwa na maono ya kuwakwamua wananchi kiuchumi kwani Mkoa wa Dar es Salaam uko tayari katika kutekeleza programu hii ya IMASA inayolenga kutambua na kuwezesha shughuli za Kiuchumi na ukizingatia Dar es Salaam ni Mkoa wenye fursa za kiuchumi na uwezeshaji wa wanawake kiuchumi hivyo kuja kwa programu hii katika Mkoa wetu ni fursa kwetu hivyo ninawahakikishia ushirikiano katika kutekeleza mpango huu na nitoe wito kwa wanawake na makundi maalumu  kushiriki kikamilifu katika hili kwani huu ni wakati muafaka kwenu wa kujikwamua kiuchumi”.

Naye, Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) Bi. Bengi Issa ameeleza kuwa  mpango huo unafungua milango kwa wanawake kutambulika rasmi wao na biashara zao na mahali wanapofanyia shughuli zao za kibiashara kwani biashara nyingi ndogondogo za wanawake sio rasmi na wengi hawana leseni hivyo kupitia mpango huu wanawake watawaweza kujikwamua kiuchumi kwani watapatiwa mikopo kwaajili ya kukuza mitaji yao.

“Pamoja na mambo mengine mpango huo utaweza kutengeneza kanzidata ya kupata takwimu za wanawake hapa nchini na hizo ni juhudi za Serikali za kuanzisha programu hii ambayo itasimamiwa na baraza ili kuweza kuwapa elimu kuhusu mambo ya kodi, biashara , ujasiriamali , kanuni na sheria mbalimbali hapa nchini”. amesema Bi. Issa






Matangazo

  • TAARIFA KWA UMMA February 19, 2025
  • TAARIFA KWA UMMA - MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA January 17, 2025
  • MATOKEO YA UPIMAJI WA KITAIFA WA DARASA LA NNE (SFNA) 2024 January 04, 2025
  • UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA, 2025 December 16, 2024
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • "Tutahakikisha tunasimamia Kata 36 na Mitaa 159 ili Jiji la DSM liwe safi" - DC Mpogolo

    May 03, 2025
  • Jiji La DSM laweka mikakati kushinda UMITASHUMTA ngazi ya Mkoa

    April 29, 2025
  • Wakazi wa Jiji la Dar es Salaam waadhimisha Muungano kwa kupanda miti na kufanya usafi wa mazingira

    April 26, 2025
  • Zoezi la usafi wa mwisho wa wiki laendelea

    April 12, 2025
  • Angalia zote

Video

Msimbazi Basin Development Project Implementation Area
Video Zingine

Viunganishi vya Haraka

  • Mameya wa zamani wa Jiji
  • Vibali vya kuingia na Pikipiki katikati ya Jiji
  • Udhibiti wa Taka ngumu Jijini
  • Eneo Maalum la Usafi Jijini
  • Kituo cha Urithi wa Ubunifu Majengo na Utalii
  • Uwanda wa Bahari, Fukwe na Visiwa
  • Sehemu za Kitamaduni, Ngoma za Asili na Sanaa za Mikono
  • Majengo na Maeneo ya Kihistoria
  • Maeneo ya Kupumzika, Bustani na Viwanja vya Michezo

Viunganishi Linganifu

  • BUNGE
  • Blogu ya Jiji
  • UTUMISHI
  • IKULU
  • TAMISEMI
  • IDARA YA HABARI MAELEZO

Wasomaji mbalimbali duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM

    Anuani ya Posta: S.L.P 20950

    Simu ya mezani: 0738 378 386

    Namba ya Mkononi: 0738 378 386

    Barua Pepe: info@dcc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.