• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Dar es Salaam City Council
Dar es Salaam City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Jiji
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Fedha, Utawala na Utumishi
      • Ujenzi na Zimamoto
      • Udhibiti Taka
      • Mipangomiji, Mazingira na Usafirishaji
      • Afya na Huduma za Tiba
    • Vitengo
      • Mipango, Ufuatiliaji na Takwimu
      • Sheria na Usalama
      • Itifaki, Uhusiano na Umma
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Ugavi na Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Shughuli za Utalii
      • Dar es Salaam Yetu
      • Misitu na Mashamba ya wanyama wafugwao
      • Sehemu za kitamaduni, ngoma za asili na sanaa za mikono
      • Kituo cha Urithi wa Ubunifu Majengo na Utalii
      • Maeneo ya kupumzika, bustani na viwanja vya michezo
      • Maeneo ya Manunuzi
      • Majengo na maeneo ya kihistoria
      • Uwanda wa bahari, fukwe na visiwa
    • Urejelezaji wa Taka Ngumu
  • Huduma Zetu
    • Vibali vya Pikipiki
    • Vibali vya Maegesho ya Teksi
    • Vibali vya Kuingiza Magari ya Mizigo
    • Vituo Vikuu vya Mabasi
    • Udhibiti Taka Ngumu
    • Taarifa za Historia ya Viwanja
    • Mazishi ya miili ya marehemu wasiokuwa na ndugu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha na Uongozi
      • Kamati ya Mipangomiji, Mazingira na Miundombinu
      • Kamati ya Mipango na Ufuatiliaji
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba ya Vikao vya Kisheria
    • Ratiba ya Mstahiki Meya
    • Mameya Wazamani wa Jiji
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi iliyo kwenye Mpango
    • Miradi Inayoendelea
    • Vitega Uchumi vya Jiji
  • Machapisho
    • Sheria
    • Sheria Ndogo
    • Sera
    • Miongozo
    • Taarifa mbalimbali
    • Fomu za Maombi
    • Fomu za Ahadi ya Uadilifu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Hotuba
    • Habari Mpya
    • Matukio

Wataalamu Kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji wafanya ziara ya mafunzo Jiji la DSM

Tarehe iliyowekwa: August 23rd, 2024

Wataalamu kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji leo tarehe 23 Agosti, 2024 wamefanya ziara katika Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kwa lengo la kujifunza na kubadilishana uzoefu katika eneo la ukusanyaji wa mapato pamoja na utekelezaji wa miradi.

Wakiwa katika Ukumbi wa Mikutano wa Arnatoglou Jijini humo, Wataalumu hao waliweza kujifunza namna mbalilimbali  Jiji la Dar es Salaam linavyofanya kazi zake katika eneo la ukusanyaji wa mapato pamoja na kujifunza mbinu mbalimbali za kuongeza mapato pamoja na kusimamia miradi kwani kwa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam mapato yameongezeka kwa kasi kutokana na kuanzishwa kwa kanda za huduma ambazo zimekua chachu ya ongezeko la asimia 105% ya mapato ya ndani ya Halmashauri ukilinganisha na mwaka 2022/2023.

Akiongea wakati wa Mafunzo, hayo Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam Ndg. Elihuruma Mabelya ameeleza kuwa “Napenda kushukuru ujio wenu kwani Ujumbe huu unaonesha jinsi gani Jiji la Dar es Salaam tumejiimarisha katika eneo la ukusanyaji wa Mapato hadi kuwa kivutio kwa wengine kujifunza kwetu  hivyo kipekee napenda kutoa Shukrani kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa fedha anazoendelea kuzileta Jijini kwetu za utekelezaji wa Miradi pamoja na Madiwani wa Jiji la Dar es Salaam ambao wao ndio wasimamizi wakuu wa miradi hii kwakua ni wenyeviti wa mabaraza ya maendeleo ya Kata wamekua wakishirikiana na Sisi pamoja na wataalamu wote kuhakikisha mapato yanaongezeka na miradi inatekelezwa kwa Wakati hii ikiwa ni kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora na kwa wakati hivyo niwaombe Wataalamu kutoka Rufiji mkatekeleze vyote mlivyojifunza bila kusahau ushirikiano na viongozi wenu hususani Madiwani kwao bila hao mafanikio hayawezi kuja kirahisi.”

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji Bw. Sebastian Gaganija ambaye ni Mkuu wa Kitengo cha Usafi na Uthibiti wa Taka Ngumu amempongeza Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam pamoja na   watendaji wote kwa kuweza kushirikiana vyema katika kukuza mapato ya Jiji pamoja na uaimamizi na utekelezaji  mzuri wa miradi huku akiahidi kwenda kufanyia kazi yote waliyojifunza. 

“Kwa hakika sisi kama Watendaji wa Halmashauri kwa niaba ya Mkurugenzi wetu na watendaji wote tunaishukuru sana Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kwa ziara hii tumejifunza vya kutosha na tunaimani tumebadilishana uzoefu vya kutosha na kuweza kuyafanyia kazi tukirudi Rufiji. Pia Nachukua nafasi hii kuipongeza Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa fedha kwaajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ambayo ni chachu ya maendeleo kwa nchi yetu.” Amesema Bw. Gaganija.

Aidha, Wataalamu  hao Waliweza kutembelea Soko la Kimataifa la Samaki Feri pamoja na Soko la Kisutu kujifunza namna Jiji la Dar es Salaam linavyoendesha masoko hayo katika kuhakikisha mapato yanaongezeka.

Matangazo

  • TAARIFA KWA UMMA February 19, 2025
  • TAARIFA KWA UMMA - MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA January 17, 2025
  • MATOKEO YA UPIMAJI WA KITAIFA WA DARASA LA NNE (SFNA) 2024 January 04, 2025
  • UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA, 2025 December 16, 2024
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • "Tutahakikisha tunasimamia Kata 36 na Mitaa 159 ili Jiji la DSM liwe safi" - DC Mpogolo

    May 03, 2025
  • Jiji La DSM laweka mikakati kushinda UMITASHUMTA ngazi ya Mkoa

    April 29, 2025
  • Wakazi wa Jiji la Dar es Salaam waadhimisha Muungano kwa kupanda miti na kufanya usafi wa mazingira

    April 26, 2025
  • Zoezi la usafi wa mwisho wa wiki laendelea

    April 12, 2025
  • Angalia zote

Video

Msimbazi Basin Development Project Implementation Area
Video Zingine

Viunganishi vya Haraka

  • Mameya wa zamani wa Jiji
  • Vibali vya kuingia na Pikipiki katikati ya Jiji
  • Udhibiti wa Taka ngumu Jijini
  • Eneo Maalum la Usafi Jijini
  • Kituo cha Urithi wa Ubunifu Majengo na Utalii
  • Uwanda wa Bahari, Fukwe na Visiwa
  • Sehemu za Kitamaduni, Ngoma za Asili na Sanaa za Mikono
  • Majengo na Maeneo ya Kihistoria
  • Maeneo ya Kupumzika, Bustani na Viwanja vya Michezo

Viunganishi Linganifu

  • BUNGE
  • Blogu ya Jiji
  • UTUMISHI
  • IKULU
  • TAMISEMI
  • IDARA YA HABARI MAELEZO

Wasomaji mbalimbali duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM

    Anuani ya Posta: S.L.P 20950

    Simu ya mezani: 0738 378 386

    Namba ya Mkononi: 0738 378 386

    Barua Pepe: info@dcc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.