Na: Shalua Mpanda
Baadhi ya wakuu wa Idara wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam wametembelea miradi mbalimbali ya maendeleo katika Jiji hili kujionea namna miradi hiyo inavyotekelezwa.
Akizungumza wakati wa ziara hiyo iliyofanyika Jumamosi ya tarehe 1 Februari, 2025 mkuu wa msafara huo ndugu Bernard Kishamba ambaye pia ni Mchumi anayeshughulikia masuala ya Tathmini na Ufuatiliaji ametoa wito kwa wakandarasi waliopata nafasi ya kutekeleza miradi hiyo ya maendeleo kufuata taratibu za mikataba yao na kukamilisha kwa wakati.
Baadhi ya miradi iliyotembelewa na kukaguliwa ni pamoja na ujenzi wa madarasa 7 shule ya msingi Kiyombo Mpera unaojunuisha matundu 10 ya vyoo,madawati 133 vyote vikiwa na gharama ya Shilingi milioni 180.
Mradi mwingine uliokaguliwa ni ujenzi wa vyumba vinne na matundu 15 katika shule ya Msingi Viwege unaotekelezwa kwa fedha za mapato yatokanayo na makusanyi ya ndani ya Halmashauri.
Aidha, timu hiyo kutoka Halmashauri ya Jiji ilitembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa shule ya sekondari ya ghorofa ya Kitunda Relini sambamba na nyumba ya walimu inayohengwa katika eneo hilo.
Ziara hiyo ilihitimishwa kwa kukagua eneo la kupumzika kwa ndugu wa marehemu wanaokuja kuchukua miili ya ndugu zao (mochwari) katika Kituo cha Afya Chanika.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Anuani ya Posta: S.L.P 20950
Simu ya mezani: 0738 378 386
Namba ya Mkononi: 0738 378 386
Barua Pepe: info@dcc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.