Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam leo tarehe 30 Novemba 2022 limeweza kukamilisha mafunzo ya ufahamu wa mfumo wa kujisajili vikundi kwa wenyeviti na watendaji wa mtaa kutoka jimbo la Segerea, mfumo huu ni maalumu kwa vijana, wanawake na watu wenye ulemavu ambapo Mikopo hiyo inatolewa na Halmashauri kutoka katika asilimia kumi ya mapato ya ndani ya Halmashauri kuweza kujisajili wakati wa kuomba mikopo.
Huu ni mwendelezo kwa Jimbo la Segerea ambapo siku ya tarehe 28 ilikua Jimbo la Ukonga na tarehe 29 jimbo la Ilala kikao hiki kimefanyika katika ukumbi wa Mikutano Anatoglou uliopo Mnazi Mmoja Dar es Salaam.
Akiwasilisha mada na taarifa juu ya vikundi mbalimbali ambavyo tayari vimechukua mkopo,Mkuu wa kamati ya Ufuatiliaji urejeshwaji wa mikopo Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaaam Bibi Margaresa Mazwile amesema. “Ushiriki wenu wenyeviti na watendaji wa mtaa ni kushirikiana na nyinyi katika kufuatilia marejesho ya mikopo hii kutoka kwa wananchi waweze kurejesha kwa sababu kulipa kwao kunaongeza nafasi na kukuza wigo wa kuzidi kukopesha vikundi vingine ambavyo vinasubiri mkopo”
Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam inatekeleza maagizo haya ya utoaji mkopo kwa wananchi kwa kiwango kikubwa na cha kuridhisha hivyo basi kimeandaa mpango mkakati wa kuweza kuwa bega kwa bega na wanyeviti na watendaji wote katika majimbo yote matatu yaliopo ndani ya Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam ili kuweza kufuatilia mikopo hii kukuza ushirikiano kwa viongozi hawa wa chini utadumishwa daima.
Akiongea Mwenyekiti wa kikao hiki kati ya kamati ya maendeleo ya jamii kutoka Ofisi ya Mkurugenzi na watendaji wa mtaa na wenyeviti bwana George S. Mtambalike ambaye pia ni mwenyekiti wa wenyeviti Jimbo la Segerea amesema
“Tunashukuru kwa mafunzo haya ya ufahamu katika mfumo huu Pamoja na kutambua taratibu zote za uombaji wa mikopo tunahaidi ushirikiano wetu kwenu na ushirikiano huu uanzie huku chini tutafanikiwa”.
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Anuani ya Posta: S.L.P 20950
Simu ya mezani: 0738 378 386
Namba ya Mkononi: 0738 378 386
Barua Pepe: info@dcc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.