Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kupitia Kitengo TEHAMA leo Machi 31, 2023 wametoa mafunzo ya mifumo ya ukusanyaji wa mapato kwa kutumia mfumo wa TAUSI ambao ulianza kutumika Novemba,2022.
Mafunzo hayo yaliyofanyika katika Ukumbi wa Arnatoglou Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam yaliweza kuhudhuriwa na Watendaji Kata wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam ambapo Mada tatu ziliweza kuwasilishwa ikiwa ni sehemu ya kuwajengea uwezo watendaji hao kuelewa mfumo huo, aidha mada hizo ilikua ni pamoja na Kufugwa kwa mfumo ww ukusanyaji wa ukusanyaji Mapato wa LGRCIS, mfumo mpya wa ukusanyaji wa mapato wa TAUSI pamoja na mfumo wa ukusanyaji mapato TERMIS (Maegesho).
Akiongoza mafunzo hayo kwa niaba ya Muweka Hazina wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salam Msimamizi wa Mapato wa Halmashauri ya Jiji Bw.Thomas Shingi amesema “Niwashukuru kwa kuja kwenye mafunzo haya ya kukuza ongezeko la ukusanyaji wa mapato katika Halmashauri yetu kwani kutokana na mlichojifunza leo naamini mtakua wasimamismizi wazuri wa mfumo wa TAUSI kwa wakusanyaji wa mapato wa Kata zenu pia ikitoke kuna changamoto yoyote linabidi mtushirikishe sisi ili tuweze kutatua tatizo hilo na kuhakikisha tunakusanya mapato kwa wingi.”
Aidha Bw.Shingi ameendelea kusema “Kutokana na ulinzinuliowekwa katika mfumo huu natoa wito kwenu muhakikishe wafanya biashara wote wanajisajili kwenye mfumo,msibe mianya ya rusha katika ukusanyaji wa mapato hivyo naamini kwa mafuzo mliyoyapata mtaenda kutekeleza vyema majukumu yenu kwa kiasi kikubwa na ongezeko la ukusanyaji wa mapato litaongezeka kwa kiwango cha juu kabisa.”
Akitoa mafunzo hayo Afisa TEHAMA wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Bi. Neema Ngavatula ameeleza kuwa kutokana na changamoto zilizobainiwa na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) katika mfumo wa kielektroniki wa ukusanyaji wa mapato LGRCIS uliokua ukitumika mwaka wa fedha 2014/2015 kutoendana na mabadiliko ya sayansi na teknolojia ililazimika mfumo huo kufungwa mwaka wa fedha 2022/2023 na hivyo kuanzishwa mfumo Mpya wa TAUSI.
“Mfumo huu mpya wa TAUSI ambao huendana na kasi ya teknolojia huishi hadi miakoa 20 ikiwa ni kipindi cha muda mrefu ambapo pia mfumo huu huweza kugundua hatari kwa haraka na kuzuia kwa haraka huku ukiweza kumsaidia mteja kujihudumia kupitia dirisha la mteja (Taxpayer Portal) ambapo mteja ataweza kulipa tozo, ushuru, leseni, faini pamoja na vibali mbalimbali bila kufika ofisi za mapato za Halmashauri.” Ameeleza Bi.Neema
Sambamba na hilo mfumo wa TAUSI unaweza kumsaidia mwananchi kujihudumia mwenyewe pindi anapotaka kuanzisha biashara kwani ataweza kutumia simu yake ya mkononi kujisajili katika mfumo na atapata huduma zote kadiri ya anavyohitaji kwa kutumia kiunganishi(Link) ‘tausi.tamisemi.go.tz.’
Akiendelea kutoa Mafunzo hayo Afisa TEHAMA Bw. Ezekia Pwele ameeleza kuwa mfumo wa mapato kutoka chanzo cha maegesho Mfumo ni mfumo ambao ulikua ukitumiwa na wakala wa Barabara za Mjininna Vijijini (TARURA ) hivyo baada Mfumo huu kukabidhiwa kwenye halmashauri inawalizimu kutoa mafunzo kwa wananchi ili waweze kujua kuhusu mfumo huu kwani ikitoke mwananchi kakutwa na kosa la kuegesha garinsehemu isiyoruhusiwa itawawezesha wakusanyaji wa mapato ya maegesho kupiga picha namba za gari na moja kwa moja ataandikiwa deni lake na ujumbe mfupi utamfikia na namna atakavyotakiwa kulipa deni.
Aidha Mwananchi kwa kutumia namba ya gari anaweza kutumia mfumo huo kuangalia deni lake au kulipa deni kwa kutumia kiunganishi (Link) ‘ termis.tarura.go.tz’
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Anuani ya Posta: S.L.P 20950
Simu ya mezani: 0738 378 386
Namba ya Mkononi: 0738 378 386
Barua Pepe: info@dcc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.