Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Amos Makalla amewataka wazazi Jijini humo kuhakikisha wanawaandaa watoto wao kujiunga Shule ya awali, darasa la kwanza na pia kidato Cha kwanza na kwakua Serikali imefanya Jitihada kubwa za kujenga miundombinu ya madarasa Kwa ajili ya wanafunzi kupata Elimu bora .
Mhe. Makalla ameyasema hayo alipofanya Ziara ya ukaguzi wa Maendeleo ya Ujenzi wa vyumba vya Madarasa 310 vinavyojengwa katika Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam ambapo jumla ya shilingi bilioni 6.2 zimetolewa Kwa ajili ya Ujenzi wa Madarasa hayo .
Aidha, Mhe. Makalla amemshukuru Mhe. Rais Dkt Samia Suluhu Hassan Kwa nia yake ya kuondoa kero ya upungufu wa Madarasa ambao utaondoa kero ya Michango Kwa wazazi ambapo Mkoa wa Dar es Salaam umewezeshwa jumla ya shilingi Bilioni 12 Kwa Ajili ya Ujenzi wa Madarasa hayo.
"Miaka Yote Kila inapofika Mwisho wa Mwaka tumekua Kama zimamoto kutafuta Fedha za Kujenga Madarasa lakini Mwaka Jana na Mwaka huu Dkt. Samia ametuondolea changamoto hiyo Kwa kutupa Fedha
“Naipongeza Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Chini ya Kaimu Mkurugenzi . Nimeridhishwa sana kuona Kati ya vyumba 310 vinavyojengwa Mpaka Sasa Kuna vyumba 220 vipo hatua yya uwezekaji Hongereni Sana " alisema Mhe. Makalla
Awali akiwasilisha taarifa ya Maendeleo ya Ujenzi, Kaimu Mkurugenzi wa Jiji Mhahindisi Amani Mfuru amesema kuwa Idadi ya wanafunzi wanaotarajiwa kujiunga Shule ya awali ni 5700, darasa la kwanza 25, 400 huku kidato cha kwanza wanafunzi 30,500 .
1 BARABARA YA MOROGORO 11882 DAR ES SALAAM
Anuani ya Posta: S.L.P 20950
Simu ya mezani: 0738 378 386
Namba ya Mkononi: 0738 378 386
Barua Pepe: info@dcc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. Haki Zote Zimehifadhiwa.